Jinsi nilivyowahi kutapeliwa na wana-JF

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
8,468
14,960
Habarini. Kama ilivyo mitandao mingine, JF nayo ina watu wa kila aina kuna wema na wabaya. Waungwana na washenzi. Binafsi humu JF nimefanya kazi na watu wengi sana. Wengi ni waaminifu na tulifanya kazi safi. Ila pia kuna matapeli. Nitaweka visa viwili vya kutapeliwa na wana JF.

1. Kisa cha kwanza ni cha "Ngosha." hiki kilitokea muda mrefu sana hata sikumbuki ni nani alikuwa na ID ile. Kuna jamaa aliweka uzi wa group la whatsapp la kusoma vitabu na link. Nikajiunga. Nikakuta humo ndani member kadhaa. Huyu jamaa namwita Ngosha sababu alijitambulisha ni msukuma yuko Mwanza. Group lilikuwa zuri na vitabu vilijadiliwa. Huyu admin, Ngosha alikuwa anastori flani nyingi kama mtu matawi. Siku moja akaja DM anaazima 20k amepungukiwa mafuta ya gari anataka kuwahi Shinyanga kumuona mama yake mgonjwa. Nikamwambia sina, maana nilianza kuona utapeli huu. Siku nyingine akaja tena DM akidai sijui kapungukiwa nini, nikamwambia sina. Akaacha kunitafuta.

kuna siku tukawa tunajadili kwenye group nikawa nimegusia kuagiza amazon vitabu fulani. Ngosha akaja DM na kusema kuwa huwa anaagiza sana vitabu. Tukiagiza pamoja itakuwa rahisi. Nikaona fresh tufanye kuagiza pamoja. Gharama yangu ilikuwa kama 80. Nikamtumia admin Ngosha ili alipie anakoagizaga. Siku ya vitabu kufika akaanza za nimeenda Kenya. Jamaa yangu huyu mcheki atakutumia. Namcheki jaamaa anasema nimtumie 10,000 ya kusafirisha. Nikatuma. Najiamini ngosha tupo naye kwa group na kila mtu aliona tunagusia kuagiza vitabu pamoja. Basi ile tena ndiyo ikawa mwisho wa kupatikana kwa Ngosha aliyeenda "Kenya" na jamaa yake. Nikampigia mdau wa kwenye group akasema "Na mimi alikuwa akinifuata fuata sana DM kuomba hela." Nikawataarifu wana group kuwa Ngosha ni tapeli. Mara admin akaleft group(nilicheka sana hii scenario ya admin kuleft!!) japo nadhani atakuwa alikuwa na account nyingine. Baadaye nikaleft lile group.

2. Kisa cha pili ni hawa jamaa wanaitwa Jibebe Inc @bluehost agent Tanzania au Kazi host. ni developers. Tunatengeneza na Kudesign logo, Business card, Websites Pamoja na Android Application
Nina side hustle ya app ya kusomea vitabu. Sasa katika kutafuta developer wa kutengeneza app nikakutana na uzi wa hawa jamaa. Nikawasiliana nao. Tukakubaliana bei ya kuunda app na domain na hosting. Ukweli jamaa waliunda app nzuri na fasta sana ila pesa mbele sana, bila pesa hata simu hawapokei. Fast forward, jamaa baada ya mwaka ukafika wakati wa kulipia hosting na domain. Jumla 120,000. Nikawalipa jamaa pesa yao. Hiyo ni kama mwezi wa nane mwaka huu. Jamaa wakapokea pesa na hosting hawajalipia. Mwisho wa siku app ikazima. Raia waliosubscribe kwa mwaka na miezi sita wakaanza kuniona siyo. Jamaa kuwauliza shida nini, habari zinakuwa nyingi. Mwisho wakaacha kupokea simu wala kujibu msg. Leo hii zaidi ya miezi miwili jamaa wamekula 120, app imezima na wala hawapokei simu. Jamaa app wanaunda vizuri, ila kama unafanya nao kazi nashauri usihost kwao, kitengo hicho watakutapeli.

Basi hivyo ndivyo nilivyopigwa na wana JF:)
 
Habarini. Kama ilivyo mitandao mingine, JF nayo ina watu wa kila aina kuna wema na wabaya. Waungwana na washenzi. Binafsi humu JF nimefanya kazi na watu wengi sana. Wengi ni waaminifu na tulifanya kazi safi. Ila pia kuna matapeli. Nitaweka visa viwili vya kutapeliwa na wana JF.

1. Kisa cha kwanza ni cha "Ngosha." hiki kilitokea muda mrefu sana hata sikumbuki ni nani alikuwa na ID ile. Kuna jamaa aliweka uzi wa group la whatsapp la kusoma vitabu na link. Nikajiunga. Nikakuta humo ndani member kadhaa. Huyu jamaa namwita Ngosha sababu alijitambulisha ni msukuma yuko Mwanza. Group lilikuwa zuri na vitabu vilijadiliwa. Huyu admin, Ngosha alikuwa anastori flani nyingi kama mtu matawi. Siku moja akaja DM anaazima 20k amepungukiwa mafuta ya gari anataka kuwahi Shinyanga kumuona mama yake mgonjwa. Nikamwambia sina, maana nilianza kuona utapeli huu. Siku nyingine akaja tena DM akidai sijui kapungukiwa nini, nikamwambia sina. Akaacha kunitafuta.

kuna siku tukawa tunajadili kwenye group nikawa nimegusia kuagiza amazon vitabu fulani. Ngosha akaja DM na kusema kuwa huwa anaagiza sana vitabu. Tukiagiza pamoja itakuwa rahisi. Nikaona fresh tufanye kuagiza pamoja. Gharama yangu ilikuwa kama 80. Nikamtumia admin Ngosha ili alipie anakoagizaga. Siku ya vitabu kufika akaanza za nimeenda Kenya. Jamaa yangu huyu mcheki atakutumia. Namcheki jaamaa anasema nimtumie 10,000 ya kusafirisha. Nikatuma. Najiamini ngosha tupo naye kwa group na kila mtu aliona tunagusia kuagiza vitabu pamoja. Basi ile tena ndiyo ikawa mwisho wa kupatikana kwa Ngosha aliyeenda "Kenya" na jamaa yake. Nikampigia mdau wa kwenye group akasema "Na mimi alikuwa akinifuata fuata sana DM kuomba hela." Nikawataarifu wana group kuwa Ngosha ni tapeli. Mara admin akaleft group(nilicheka sana hii scenario ya admin kuleft!!) japo nadhani atakuwa alikuwa na account nyingine. Baadaye nikaleft lile group.

2. Kisa cha pili ni hawa jamaa wanaitwa Jibebe Inc @bluehost agent Tanzania au Kazi host. ni developers. Tunatengeneza na Kudesign logo, Business card, Websites Pamoja na Android Application
Nina side hustle ya app ya kusomea vitabu. Sasa katika kutafuta developer wa kutengeneza app nikakutana na uzi wa hawa jamaa. Nikawasiliana nao. Tukakubaliana bei ya kuunda app na domain na hosting. Ukweli jamaa waliunda app nzuri na fasta sana ila pesa mbele sana, bila pesa hata simu hawapokei. Fast forward, jamaa baada ya mwaka ukafika wakati wa kulipia hosting na domain. Jumla 120,000. Nikawalipa jamaa pesa yao. Hiyo ni kama mwezi wa nane mwaka huu. Jamaa wakapokea pesa na hosting hawajalipia. Mwisho wa siku app ikazima. Raia waliosubscribe kwa mwaka na miezi sita wakaanza kuniona siyo. Jamaa kuwauliza shida nini, habari zinakuwa nyingi. Mwisho wakaacha kuppkea simu wala kujibu msg. Leo hii zaidi ya miezi miwili jamaa wamekula 120, app imezima na wala hawapokei simu. Jamaa app wanaunda vizuri, ila kama unafanya nao kazi nashauri usihost kwao, kitengo hicho watakutapeli.

Basi hivyo ndivyo nilivyopigwa na wana JF:)
Pole sana.
 
Back
Top Bottom