Jina la ukoo lina nguvu kubwa sana kiroho

James Hadley Chase

JF-Expert Member
Mar 25, 2020
1,984
3,664
Jina la ukoo lina nguvu sana. Jina la ukoo Sio jina kama unavyoliona. Ni damu ya uzao.

Hata kama umezaa na mtu na ukabadilisha jina la mtoto kisa baba yake HATOI matumizi au kisa umehangaika na MIMBA pekeako. Kumbuka damu ya mtoto NDIO imelala na jina hilo.

Vyote vinavyohusiana na mtoto huyo vitafanya kazi.

WAKATI MWINGINE mtoto anaweza kumbambika kwa baba MWINGINE ila ukoo wake unamkontrol kiroho.

Na ukoo Ukiwa na nguvu na mila za mizimu na kiroho BASI mtoto ATAKUWA na mambo ya HOVYO.

Kuumwa HOVYO.
Kulia HOVYO
Jeuri jeuri
Hakusikilizi

Yaani ukienda shuleni HOVYO Matokeo.

Kumbe damu ya baba inatembea mwilini.

Ndio maana kuna ukoo wanasema hatupotezi mtoto.

Hata umwite jina la kwenu na kumfuta baba yake au ukoo wake basi HIYO ni vita haitamuacha mbaka anakufa.

Wengine wanapotea potea KILA SIKU kisa jina na damu ya ukoo wa baba yake.

Hata vitabu vimekataa KUBADILISHA ukoo bila sababu ya Haki.

Mtoto unapeleka hospitali mbaka unachoka. Ila SIKU ukimpeleka kwa babu yake. BASI degedege linakata hapo hapo.

Ukoo au damu ya mtoto haikatwi milele. Utabadilisha jina tu ila damu ni ile ile na itafanya kazi.
 
WAKATI MWINGINE mtoto anaweza kumbambika kwa baba MWINGINE ila ukoo wake unamkontrol kiroho.
Kuna mzee ana watoto 5, wa 4 mkewe alicheza rafu na akaficha. Ana tabia tofauti na ndugu zake, tabia zake zinafanania koo ya baba yake halisi(haishi mbali). Kwenye utafutaji na mafanikio anapitia wanayopitia koo halisi ya baba yake lakini hawa ndugu zake wanne ni tofauti kabisa.
 
mmmh kila nikijaribu kusoma hichi kitu naambulia patupu hapa ulikuwa unasemaje mku?😂
 
Back
Top Bottom