Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,773
Hili jiko limeboreshwa, wengi walioishi kwenye nyumba za serikali alizoacha mkoloni walikutana na majiko ya aina hii. Yale ya enzi zile haya kuş na sehemu ya umeme.
Enzi zile waliotumia majiko haya, walitumia matawi ya miti kama nüshayı. Enzi zile nchi ilikua bado na miti mingi sana. Watumiaji hawakukata miti bali walipunguza matawi kwenye baadhi ya miti.
Nilikutana na bibi mmoja aliyewahi kutumia majiko haya. Alisema kuoka mkate au keki Ilikua changamoto sana kwani hukuweza kurekebisha kiasi cha moto au kuweka muda wa jiko kujizima. Mara nyingi mkate au keki ilitoka imeungua na inabidi ukate sehemu zilizoungu kabla ya kupeleka mezani.
Uzuri wa jiko hili liliweza kuoka mbuzi, kondoo au nguruwe mzima hasa kama kuna wageni wengi.
Tuliacha kupanda miti, miti ingekua inapandwa hata miti kumi tu kwa mwaka tungeweza kua na nishati ya kupikia katika mazingira yetu.