Jiji la Arusha majuto matupu, ufisadi wa madiwani wa CCM unaimaliza halmashauri

Tanzaoregano

New Member
Aug 31, 2022
3
1
aada ya CCM kupora uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 na kuongoza halmashauri, wananchi wa Jiji la Arusha tunasikitika kuona mbunge na madiwani wake wamesahau jukumu la kuwaletea wananchi maendeleo na kujikita katika upigaji wa madili ya kifisadi ili kushibisha matumbo yao bila kujali maumivu ya wanaowaongoza.

Kabla hatujasahau kashfa kubwa ya ufisadi iliyolikumba Jiji hilo na kupelekea baadhi ya viongozi wake kuswekwa korokoroni wakituhumiwa kwa ubadhirifu wa mamilioni ya fedha za wananchi wanyonge, madiwani wa CCM wanatuhumiwa kuchukua rushwa ili kumlinda mfanyabiashara maarufu Jijini Arusha anayemiliki kampuni ya utalii ya Leopard Tours ambaye amejenga ofisi yake katika hifadhi ya barabara ya Kijenge. Mfanyabiashara huyu amegeuka shamba kwa madiwani wa CCM pamoja maafisa wa TANROADS ili kumlinda mfanyabiashara huyo.

Diwani wa viti maalumu Blandina, diwani wa Sinon Mzee Kivuyo, diwani wa Kimandolu Kobra pamoja na wenzao walichukua rushwa ya Tsh. 5,000,000/= toka kwa Leopard Tours na kwenda kugawana katika bar ya Kipong. Viwango tofautitofauti vya milioni 30, 60 na 145 viliendelea kutolewa kwa nyakati tofauti tofauti.

Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Maxmillian Iranqhe yeye alipokea Doller 2000 pale Kibo Palace Hotel. Diwani wa Lemara ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mipangomiji Mhe Naboti yupo kwenye kampeni ya kumshawishi mhindi wa Leopard aongeze fedha ili halmashauri imuuzie eneo hilo. Ikumbukwe beacon ya mpaka wa hifadhi ya barabara husika imejengewa ndani ya ukuta wa ofisi ya Leopard tours.

Eneo hili lilipaswa kuhifadhiwa kama sheria inavyoelekeza ama kama anakodishiwa alipe kodi serikalini.
Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo amelikalia kimya jambo hili kwa kuwa ni rafiki mkubwa wa wafanyabiashara wa kihindi na baadhi ya madiwani waliotajwa katika kashfa hii.

Arusha tunaumizwa na tozo pamoja na ufisadi wa baraza la madiwani, Mama Samia tupia jicho Jiji la Arusha, maelekezo ya kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake yameeleweka Arusha. Kwa uhuni huu wa CCM Arusha 2025 mfungashe virago vyenu.
 
Meya mbona kapokea mgawo mdogo sana? $2000 ni ndogo sana kiasi cha kujichafua.
 
Back
Top Bottom