Jihadhari na utapeli wa kupatiwa ajira

KATI 2

JF-Expert Member
Dec 14, 2012
214
20
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI


KUIBUBUKA KWA MAKUNDI YA UTAPELI.

Katika siku za hivi karibuni katika maeneo mbalimbali hapa nchini, kumejitokeza makundi ya watu ama mtu binafsi kutumia mwamvuri wa taasisi fulani kujipatia kipato kwa njia za udanganyifu (utapeli) kwa kuwaahidi vijana kwamba watawapatia ajira katika taasisi hizo.

Makundi haya ya kihalifu imebainika kwamba yapo katika maeneo mbalimbali, hivyo, ni suala ambalo linahitaji ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi ili kukomesha vitendo hivyo. Juhudi za makusudi zinaendelea kufanyika na jeshi la polisi ili kuwatia mbaroni watu wote wanaojihusisha na vitendo hivyo vya kitapeli.

Aidha, kufuatia kuibuka kwa vitendo hivyo, tayari Jeshi la Polisi limewakamata matapeli wawili wakiwa wamekusanya vijana katika mikoa ya Kilimanjaro na Mbeya, uchunguzi dhidi yao unaendelea na pindi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabiri.

Jeshi la Polisi likishirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama, kimsingi, kazi yetu kubwa ni kuhakikisha Tanzania inakuwa na Ulinzi na Usalama imara. Tutaendelea kupambana na makundi haya ya kihalifu na utapeli ili nchi yetu iendelee kuwa salama.

Tunawasihi wananchi kufuatilia taarifa kwenye vyanzo sahihi juu ya jambo lolote wanalotaka kulifanya ili kuepuka utapeli unaoweza kufanywa na baadhi ya watu kwa lengo la kujipatia vipato. Aidha, wananchi watoe taarifa kwenye vyombo vya usalama kuhusu tabia na mienendo yoyote wanayoitilia mashaka. Jeshi la Polisi na vyombo vingine vyote vya Ulinzi na Usalama viko imara, makundi ya kiuhalifu na wahalifu wote wajue hawana pa kukimbilia, watakamatwa.


Imetolewa na:
Advera John Bulimba – SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu ya Polisi.
14/04/2016
 
Hizi habari zienezwe kila mahali kwakuwa kwenye sekta hii wanaoumizwa ni wengi kila mwaka
 
Mbona hata humu JF wamo wengi tu
Hasa wale wazee wa Utajiri wa Mtandao,yaani uwe na Computer tu unakuwa Tajiri.
Aiseee
 
Ishu ya mkataba wa Lugumi vipi mama mbona nayo huitolei ufafanuzi
 
na sio wa ajira tuu kuna ht wale wanaopga cm kujifanya wanakujua af wanakupa dili la kununua vifaa flan
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…