matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,634
- 18,541
Mwanzo 15, Ibrahim alielekezwa na Mungu atoe sadaka ili apate kuhakikishiwa hatma ya maisha yake.
Aliziandaa akazilinda hadi jioni tai na mbwa mwitu wasije wakazitafuna. Alifanikiwa hadi jioni mpaka zilipoleta matokeo.
Watu wengi hawanufaiki na sadaka zao kwa sababu hawazilindi. Wanatoa kama wanazitupa tu.
JINSI YA KUZILINDA SADAKA ZAKO.
1: Usitoe sadaka kisha ukaondoka. Jifunze kulinda kwa kuzitamkia maneno ambayo unataka Mungu akufanyie. Hata kama unampa ombaomba mtaani, kabla hujatoa tamka.
2: Usitoe mahala unapopatilia mashaka. Usitoe kwa mtumishi unayemtilia shaka au unauhakika atazifuja na Mungu ameshakuonyesha. Toa mahala ambapo moyo wako hauna tashwishwi. Mungu hampendi mtu mwenye mashaka na wasiwasi.
3: Usitoe kwa kulazimishwa. Kanisani hakuna michango. Kila kitu ni sadaka. Ukitoa kwa lazima uhakikishe ni matokeo ya maamuzi yako sio manipulation au janjajanja ya mtozaji au vitisho au shuruti. Hutabarikiwa.
4: Kubwa kuliko yote, baada ya kutoa, baki ukiwa unaendelea kujitamkia maneno chanya ukiendeleza yale uliyotamka wakati unatoa. Ukijikuta unalaumu au unalalamikia ulichotoa unajiletea laana. Endelea kuwa chanya na sadaka yako hadi kusudi ya kulitoa litakapotimia.
Ni hayo tu.
Kama umeelewa, sema amina.