Nick J Vuitton
Member
- Oct 6, 2016
- 56
- 153
Mkuu huu ugonjwa uliwahi nipata nilipulizia innovex ukaisha kabisaYes dah pole sana
Hii kwanza inasambazwa na maji sababu iko ardhini au vifaa vya shambani,jitahidi eneo ambalo limeathirika zaidi basi lipewe huduma peke yake usichanganye na eneo lingine. Jitahidi kuepuka kusababisha vidonda sababu kikitokea tu ndio hapo hapo mmea unapoanzia kuathirika jitahidi upulize dawa zenye copper zitakusaidia kuzuia maambukizi ya hewani kwa kuziba vidonda.
Kikubwa dawa hakuna ikiwa mapema unaweza tumia Trichodema ambao ni bacteria wanaokula bacteria waharibifu lakini inatakiwa ianze toka kwenye kitalu kwa sasa umechelewa.
Next time ukilima tumia mbegu inayovumilia hili tatizo kama kipato f1 ya east west seed,Tengeru 97 (sema hii ni nyanya duara) sinahakika ila ni kati ya kibo au east Africa seed
Iliyoshambuliwa ing'oe ikikaa inaendelea kuzalisha wadudu zaidi