Jeshi la polisi wamlilia Ernest Mangu

Nimeicopy kama ilivyo kutoka mtamboni......

Baada ya kufanya mahojiano na askari polisi maeneo mbalimbali ya nchi hii kwa njia ya simu kwa wale wa mbali na wale wa karibu kuongea nao ana kwa ana hasa baada ya utenguaji na uteuzi wa mkuu mpya wa polisi IGP , askari wengi ambao niwazoefu na wamefanya kazi na viongozi hawa wote wana kiri kwamba utenguzi huo umewashtua na wengi umewaumiza sana

Wanadai kwamba Mangu alikuwa mtetezi wao mkubwa sana na amewatetea askari wake walio chini yake kwa nguvu kubwa sana ikiwa ni pamoja na kuihimiza serikali kuwaboreshea maslahi yao na mahitaji yao mbalimbali, ingawa kuna baadhi serikali ilikuwa ikilega lega kuyatimiza lakini Mangu alijitahidi sana kufuatilia.

Lakin pia wamedai Mangu ni mtu mwenye misimamo dhabiti na anayejua vema kusimamia maadili na miongozo ya kazi yake kikamilifu, asiye yumbishwa , asiye ingiza siasa katika kazi au yupo radhi akae kimya na asiwe muongeaji kabisa pale anapo ona kuna mbinu zinazo kiuka madili ya kazi yake na kama mbinu hizo zipo juu ya uwezo wake kimaamuzi

"Unajua kaka huyu jamaa kwakweli sisi kama askari tulikuwa tunampenda sana maana ni kiongozi aliye kuwa akitujali sana na ametupigania sana serikalini ili tupate baadhi ya stahiki zetu kwakweli jamaa ametufaa sana ila ni basi tu kaka maana huyu mwingine kisha ingizwa kwenye siasa yaani daah sijui lakin ila nimeumia sana lakin sisi hatuna tatizo kaka sisi ni punda tu yeyote anaye kabidhiwa mjeredi kutuongoza sie tutavuta mzigo tu hahaaaa" alisikika afande mmoja akitoa yake ya moyoni huku akimalizia na kicheko

Lakin pia walio wengi wamemuongelea Sirro kuwa hana shida katika utekelezaji wa majukumu yake lakini huwa si mtu anae weza kusimamia misimamo ya kazi yake na kwa sasa amepoteza ule u Sirro aliokuwa nao hapo zamani, wamemuingiza kwenye siasa kinguvu,, ila naye si mbaya ingawa hatujui akipewa madaraka makubwa hayo atakuwaje lakin kwa hali ilivyo sasa na utawala huu wa sasa askari wengi wame hofia kufanya kazi kisiasa zaid kuliko kuzingatia kanuni ,taratibu, miiko na weledi wa kazi yako

Mada yako Ulilenga kusema kwamba kuna siasa huko kitu ambacho si kweli. Mangu alifanya wajibu wake na amemaliza muda kwa mujibu wa matakwa ya JPM ambaye ana mamlaka ya kuteua. Hao askari watulie tu na kufanya kazi zao maana mtu huwezi KUCHAGUA WAZAZI, BOSS, na Majirani. SIRO NI ASKARI - SIO MWANASIASA: SIRO ATAMUDU VIZURI JUKUMU HILO
 
Si huyu kuna wakati alidhamiria kumsweka Maalim Seif ndani mara tu akitua kutoka majuu, na huyu sharif wa Zanzibar akamwambia nitatua huko Bongo na husubutu kunishika ,Mangu akaufyata. Si alitaka kutumika kisiasa.
 
Askari nane vijana wafe hivi hivi. Amewajibika kiaina.
Huyo mkuu wa mafunzo atakuwa anahitaji semina ,
 
Nimejifunza kuwa Watanzania tuna sifa ya kuwapenda Viongozi legelege ambao wanaweza kutuvumilai tukifanya vyovyote vile, na kuwachukia Viongozi wachapa kazi.

Uyu sio mchapa kazi bali mbaguzi akikukubali ata uwe una makosa kiasi gani (mfano bashite) utabaki nafasi yako ila akikuwekea kinyongo hata uwe msafi kiasi gani ( Nape) utatumbuliwa
 
Kauli za Mangu kuhusu kutokua na maagizo kumpandisha cheo yule askari na hii ya hivi karibuni aliposema kamatakamata zinazoendelea sio msimamo wa jeshi la polisi ni baadhi ya vitu vinavyoonyesha misimamo yake.

Ana mapungufu yake, lakini hili la kutumika kisiasa amelivuka. Naona matukio mengi aliamua kutokuongea kabisa.
Mzee anataka watu wanaosema 'ndio' kama wako bungeni, hiyo ni silka ya watu wasiojiamini.
 
Back
Top Bottom