Jeshi la Polisi linataka kumpaisha kisiasa Tundu Lissu kama ambavyo walifanya Makaburu wa Afrika Kusini kwa Nelson Mandela?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,843
31,049
Tujikumbushe siasa kidogo, katika miaka ile ya 60, makaburu wa Afrika Kusini walilitumia Jeshi lao kumnyanyasa katika kila hali mzalendo wa nchi hiyo Nelson Mandela, hadi mwaka ule wa 1964, alipohukumiwa kifungo cha maisha jela, katika kesi ya kubambika ya uhaini

Nelson Mandela hakuvunjika moyo na vitendo hivyo vya kikaburu na akaendelea na msimamo wake ule ule wa kuwapigania waafrika weusi, ili wasionewe tena na watawala hao weupe wa makaburu wa Afrika Kusini

Hata hivyo pamoja na kufungwa huko kwa mwanasiasa huyo, ambako kulileta vugu vugu kubwa ambapo wananchi hao wa Afrika Kusini weusi walipaza sauti kubwa kutaka mwanasiasa huyo aachiwe huru bila masharti yoyote.

Vugu vugu lilipozidi hatimaye watawala hao wa makaburu wa Afrika Kusini walisalimu amri na kumwachia bila masharti shujaa huyo wa Afrika Kusini Nelson Mandela.

Hatimaye makaburu hao wa Afrika Kusini walisalimu amri na kumtoa jela na baada ya kutolewa jela akawa mwafrika Kusini wa kwanza mweusi kuwa Rais wa Taifa hilo la Afrika Kusini katika uchaguzi huru na wa haki na akawa ni binadamu pekee katika dunia hii kujengewa mnara katika makao makuu ya umoja wa mataifa, jijini New York, kwa kutambua mchango wake wa kijasiri mkubwa kisiasa duniani wa kupigania haki katika dunia hii na akawa ndiyo binadamu maarufu zaidi duniani aliyewahi kuishi katika karne ya 20

Turejee kwa mwanasiasa wetu Tundu Lissu, ambaye naye anafanyiwa visa mbalimbali na Jeshi la Polisi nchini vinavyofanana na visa hivyo alivyofanyiwa mzalendo huyo wa Afrika Kusini Nelson Mandela.

Kuanzia kesi za kubambika nyingi alizofunguliwa nazo katika mahakama nchini zikidaiwa kuwa ni za uchochezi, wakati kiuhalisi amekuwa akitumia haki zake za kikatiba za kukosoa utawala huu na watawala hawa wamekuwa wakikerwa na kuelezwa ukweli huo na kumfungulia kesi mfululizo hadi hatimaye kupigwa risasi mfululizo na watu ambao Jeshi letu la Polisi limekuwa likituaminisha kuwa ni watu wasiojulikana waliohusika katika jaribio hilo baya kabisa la kumwua, takribani miaka 3 iliyopita, ni miongoni ya visa anavyofanyiwa mzalendo huyu namba moja nchini kwetu.

Kitu kibaya kabisa ni hili tangazo walilolitoa Jeshi letu la Polisi kuhusu ujio wa Tundu Lissu, kuwa ni marufuku kwa wananchi kwenda kumpokea shujaa wao Tundu Lissu!

Ni kawaida kwa binadamu kuwa na shauku kubwa ya kumwona tena binadamu mwenzake ambaye amenusurika kimiujiza kama ambavyo imetokea kwa shujaa wetu Tundu Lissu, kwa hiyo ni kitendo ambacho "hakikubaliki" kwa Jeshi la Polisi, kuwakataza wananchi wasiende kumpokea shujaa wetu Tundu Lissu.

Ndipo hapo ninapojiuliza hivi Jeshi letu la Polisi linataka kumpaisha Tundu Lissu kama ambavyo Jeshi la Polisi wa makaburu wa Afrika Kusini walivyompaisha mzalendo wa nchi hiyo Nelson Mandela?
 
Kingepaa Kwanza chama Cha chadema Mana viongozi wote walikula pingu na kufanywa vilema
 
Lissu yupo angani sasa maeneo ya Egypt atatua mida ya saa saba mchana. Serikali hii na wahusika wakuu wanajichimbia makaburi yao kwa hili jambo la Lissu. Kwa vyovyote wameshindwa vibaya.
 
Kwa wananchi kumpokea ni kumfanya ajione kweli kafika nyumbani, atafarijika Sana kiukweli, Kwanza ni siku nyingi binafsi nimemmisi, polis wangewaacha wananchi wakampokee ili hamu Yao iishe

Swala moja tu ambalo wajinga na wapumbavu wengi humu wanalojidanganya, eti yeye kuwa Raisi wa nchi hii Kwa uchaguzi huu 2020/ ??

Kama kuna mtu kafanya Research ya Hilo inabidi arudishe pesa zake haraka iwezekanavyo!

Kawajaza watu matumaini ya kipumbavu kabisa
 
Kingepaa Kwanza chama Cha chadema Mana viongozi wote walikula pingu na kufanywa vilema
Nguruwe wa Lumumba mnateseka sana
Screenshot_20200628-103658.jpg
 
Lissu yupo angani sasa maeneo ya Egypt atatua mida ya saa saba mchana. Serikali hii na wahusika wakuu wanajichimbia makaburi yao kwa hili jambo la Lissu. Kwa vyovyote wameshindwa vibaya.
Kwa taarifa hiyo utasababisha baadhi ya watu wakimbizwe hospitalini kutokana na lile tatizo la "cardiac arrest" 😁 😁
 
Back
Top Bottom