Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,713
- 13,463
Jeshi la Polisi Nchini limesema hivi karibuni kumejitokeza tabia ya baadhi ya watu kujichukulia sheria mkononi kwa kufanya vitendo vya kihalifu ambavyo havikubaliki,
Akitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari leo Februari 28, 2024 Msemaji wa Jeshi la Polisi Naibu Kamishna wa Polisi DCP David Misime amesema Februari 21, 2024 huko mkoani Manyara, wilaya ya Babati, katika eneo la Magugu, wananchi wakifanya vurugu na kufunga barabara wakishinikiza Jeshi la Polisi liwakabidhi mtuhumiwa aliyekuwa akituhumiwa kumbaka kisha kumuua mtoto wa miaka saba.
Pia, DCP Misime amesema Febuari 27, 2024, mkoani Tanga katika wilaya ya Korogwe, eneo la Msambiazi, waendesha bodaboda waliteketeza kwa moto basi la Kampuni ya Sai Baba linalofanya safari zake Dar es Salaam Arusha baada ya basi hilo kumgonga dereva wa bodaboda ambaye alifariki Dunia.
Amesema Jeshi la Polisi nchini linatoa onyo kwa baadhi ya watu wanaojichukulia sheria mkononi kuacha tabia hiyo ambayo ni kinyume cha sheria na ukiukwaji wa misingi ya haki za binadamu.
Ameongeza kuwa Kitendo cha kuchoma basi kimedhulumu haki za watu wengine ambao hawakuhusika na tukio hilo la ajali.
Msemaji wa Jeshi hilo amesema Jeshi la Polisi linatoa wito kwa baadhi ya waendesha pikipiki za miguu miwili maarufu bodaboda kuacha tabia ya kujichukulia sheria Mkononi
Vilevile amesema Jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka wale wote waliohusika na uhalifu huo wa kuchoma basi Wilayani Korogwe ili wafikishwe katika vyombo vya sheria.
PIA SOMA
- Korogwe: Bodaboda wadaiwa kuchoma basi la Saibaba baada ya mwenzao kugongwa