Je, Zitto Kabwe anatumiwa na Standard Chartered Bank?

HUwezi andika makala ndefu hivi kama ama hutumiki ama hulipwi. Don't think we are all easily swayed away with easy tactics like yours!!!
Jadili hoja badala ya kumjadili mtoa hoja. Kama huna hoja nashauri ukae ukimya. Siyo lazima uandike.
 
Brother Salim Khatri live debate yako na Zitto iliishia wapi? Kama kuna mwenye feedback amwage. Muanzisha mada na ZZK ni wapinzani wakubwa kule Wanazuoni group.
Kaka, Zitto Kabwe kaniachia manyoya. Alituahidi atatuambia lini atakuwa na muda wa kushiriki huo mdahalo. Mpaka leo kaingia mitini. Labda waliokuwa karibu naye wanaweza kumuuliza lini yuko tayari kufanya huo mdahalo na mimi.

Kitu kimoja kiko wazi, Zitto Kabwe japo amekubali kufanya huo mdahalo na mimi kamwe hawezi kujitokeza. Anajua uongo wake wa PAC utawekwa hadharani na hatimaye ataumbuka. Mimi hata ukiniambia leo jioni tukafanye huo mdahalo niko tayari. Tatizo ni yeye Zitto Kabwe hayuko tayari. Aulizwe tu, nini anachokiogopa?
 
Maelezo mengi sana ila sisi wananchi wa kawaida ugomvi wetu na Escrow ni kwamba ilithibitika baadhi ya viongozi wa serikali wamepata mgawo wa pesa... tena ni mabilioni na mamiliomi ya shilingi....

Inawezekana uyo Zitto anatumika na iyo benki ya Uingereza ila ingekua vizuri zaidi ukafafanua ni vipi zile pesa walizochota akina Mh.Chenge na Tibaijuka zilihusika na hili sakata la Escrow....

Hii ni siasa kila jambo lina sura mbili mbili... hatuwezi kumhukumu Zitto kwa "unafiki" au sijui upotoshwaji wa taarifa ya kamati yake kipindi iko Halafu tukaacha kujiuliza hivi ilikuaje wale viongozi wakaingiziwa zile pesa katika akaunti zao???

Nahisi ameelewa mkuu. Wanataka kutuchanganya tusione maslahi ya taifa kwenye hili. Hii post nzima ina lengo la kumattack Zito tuu hayo maelezo mengine ni camouflage tu
 
sasa kama kamati ya PAC ilipendekeza mtambo umilikiwe na Tanzania, nashangaa unaposema zitto anatumika sasa iwapo tz itautaifisha mtambo(iptl) standard charted bank wanufaikaje wakati wao wenyewe wanataka wamiliki? yaan sjaelewa au umekuja kuwa tetea wahindi wenzio akina sethi.
 
hapo ndio anashindwa kupaelezea anabaki anazunguka tu. Pia hata uhalali wa hilo deni lenye kuwapa nguvu SCB haupo na umeshindwa kuthibitika mahakamani.
 
sasa kama kamati ya PAC ilipendekeza mtambo umilikiwe na Tanzania, nashangaa unaposema zitto anatumika sasa iwapo tz itautaifisha mtambo(iptl) standard charted bank wanufaikaje wakati wao wenyewe wanataka wamiliki? yaan sjaelewa au umekuja kuwa tetea wahindi wenzio akina sethi.
Unatakiwa kuipakua, kuisoma, na kuielewa barua ya Standard Chartered Bank. Je umeisoma na kuielewa hiyo barua?

Kwa mara ingine tena naweka tafsiri nyepesi ya masharti ya "Agreed Plan" hapa chini. Soma halafu tafakari kama jibu la swali lako lipo humo ama halipo. Zingatia sharti (b).

(a)Mchakato mzima ufanyike kupitia Bunge la Tanzania. Kutakuwa hakuna haja ya kuzihusisha mahakama kwenye hili [la kutaifisha].

(b) Upande utakaostahiki kulipwa fidia kutokanana utaifishaji huu chini ya“Makubaliano ya Hull” itakuwa wao benki [yaani SCB].

(c) Benki [SCB] itakubali masharti ya“Agreed Plan” kama ni fidia kamili (final compensation). Benki [SCB] haitajaribu kulazimisha fidia nyingine za utaifishaji ambazo zimo kwenye vipengele vya mkataba wa utekelezaji uliosaniwa Juni 8, 1995 kati ya Serikali ya Tanzania na IPTL.

(d) Benki [SCB] inakubali kutokudai, katika ngazi yoyote, kuchukua hatua yoyote katika kesi yoyote ya ICSID dhidi ya TANESCO au Serikali ya Tanzani (aidha kwa jina lake ama kwa jina la IPTL ama vinginevyo) kwenye masualayanayolalamikiwa sasa.

(e) Kutegemea muda itakapofikishwa Bungeni, “Agreed Plan” [ya kuitaifisha IPTL] unaweza kutekelezwa haraka bila ya haya ya Msimamizi ama mchakato wowote wa Mahakama.​

(unaweza kuipakua na kuisoma barua hiyo hapa:http://www.orcis.com/escrow/Letter_SCB_to_TANESCO_CEO.pdf)

Mara ya mwisho niliangalia James Rugemalira hakuwa Muhindi. Pamoja na hayo huwa sijibu hoja nyepesi na hasa hoja za kibaguzi.
 
Hivi hujui kama ripot za PAC zilikuwa mbili? Moja iliandaliwa na serikali hiyo ilikuwa batili na iliyotukuka inawapelekesha hadi leo.
 
Kaka, Zitto Kabwe kaniachia manyoya. Alituahidi atatuambia lini atakuwa na muda wa kushiriki huo mdahalo. Mpaka leo kaingia mitini. Labda waliokuwa karibu naye wanaweza kumuuliza lini yuko tayari kufanya huo mdahalo na mimi.

Kitu kimoja kiko wazi, Zitto Kabwe japo amekubali kufanya huo mdahalo na mimi kamwe hawezi kujitokeza. Anajua uongo wake wa PAC utawekwa hadharani na hatimaye ataumbuka. Mimi hata ukiniambia leo jioni tukafanye huo mdahalo niko tayari. Tatizo ni yeye Zitto Kabwe hayuko tayari. Aulizwe tu, nini anachokiogopa?

Ni nini chanzo cha kukwama pesa za mcc? Ina maana nao wazungu walikurupuka? Kwa nn walisisitiza pesa zao zingetoka hadi maazimio ya escrow ya kuwawajibisha wezi yafanyike? Na je ina maana zitto alishawishi had kamat ya mcc kuzuia zile pesa kwa kuwa katunga huo uongo?
 
Wewe mleta mada unatumika na nani????

Bottom line, Je tumeibiwa kama nchi au hatukuibiwa??? Tunastahili kulipwa au la???

Wanasiasa na waandishi wa nchi hii hawaaminiki..
 
Mleta mada haya maji marefu usipime kwa mguu wala kijiti utaendelea na kuzama.
 
Hiyo barua inadhihirisha mpango waliokuwa nao Standard Chartered Bank. Interesting enough, huo mpango ulikamilishwa kama ulivyopangwa, yaani Mahakama (zenye mamlaka ya kutoa haki) zikawekwa pembeni kama ilivyopendekezwa, Suala likapelekwa Bungeni kama ilivyopendekezwa na huo mpango, na huko suala la kutaifishwa likaletwa kama ilivyotakiwa na huo mpango wa Standard Chartered Bank. Wewe hii haikustui?

Khatri, ndugu yangu nani aliweka kando mahakama? Mahakama na Bunge ni mihimili tofauti, haiingiliani ila inaheshimiana. Bunge halina mamlaka ya kutaifisha chochote bali lina uwezo wa kuweka maazimio ambayo itayapeleka serikalini. Serikali itayaelekeza maazimio yale kwenye mamlaka husika na kuomba ushauri. Serikali haiwezi kutaifisha mali yenye umiliki halali. Wataenda Brella, TRA na kupitia hukumu za mahakama kufahamu nini la kufanya. Barua za standard chartered zisikupe shida. Inawezekana wajumbe walitumia hizo barua kama 'whistle blower mechanism', pengine bila SCB uovu usingefahamika. Kuna ubaya ganikutumia taarifa zenye kulinda maslahi ya nchi na zenye kuanika wahalifu?

Kwa mujibu wa katiba ya nchi hii, chombo pekee chenye mamlaka ya kutoa haki ni MAHAKAMA siyo BUNGE. Suala la umiliki wa IPTL unatakiwa upatiwe ufumbuzi MAHAKAMANI siyo BUNGENI. Standard Chartered Bank imetaka muhimili wa dola wenye mamlaka ya kutoa haki, yaani BUNGE iwekwe kando na badala yake suala hilo liende likaamuliwe BUNGENI.

Hoja yako kuwa kampuni inayogombewa inawezekana haina mmiliki ni hoja dhaifu kaka.

Hapa mimi ndipo nakushangaa sana kwani unalalamikia kitu ambacho hakipo. Bunge halina mamlaka ya kuipa SCB umiliki wa IPTL. Msimamo wa Bunge ni kuwa PAP ni kampuni 'famba', haipo kisheria hivyo mitambo imilikiwe na nchi na si SCB.
Sasa unavyosema kuwa SCB inataka mitambo ikitaifishwa yenyewe ndio itambuliwe kama mmiliki na kudai fidia 'nafuu' ili iikomoe PAP ndio sikuelewi. Bunge la JMT linawezaje kutoa umiliki wa IPTL kwenda kwa SCB.

Kama hoja yangu ya kuwa IPTL inagombewa kwa kuwa haina mmiliki ni dhaifu, basi wewe huna hoja. Kukosa umiliki wa kueleweka wa IPTL ndio hasa chanzo cha kuzaliwa wazo IPTL itaifishwe au wewe unafikiri wazo la kutaifisha IPTL linachagizwa na nini hasa?

Domo Kaya,
Point ni kuwa kwanini Zitto Kabwe na wenzake walikuwa wanaihodhi hiyo ripoti na kwanini hiyo Ripoti ya CAG hawakugawiwa wabunge wakati wanajadili hili suala? Kwanini Zitto Kabwe alikerwa na agizo la Rais la kutaka Ripoti ya CAG kuchapishwa kwenye magazeti ili wananchi waisome? Huoni kama kuna UHUNI ulikuwa unafanyika hapa?

Kaka nimekuuliza Zitto ana mamlaka kwenye ripoti ya CAG na CAG mwenyewe hukujibu. Sasa unarudia tena kuniambia Zitto alikerwa. Kama agizo la Rais halifanyiki kwa vile mtu mmoja anakereka hiyo ni ishu nyingine. Agizo la rais lilitekelezwa halikutekelezwa? UHUNI una tafsiri nyingi hata mwanamume aliyefikia muda wa kuoa lakini hana mke katika jamii nyingine nae huitwa muhuni, be objective!

Ugomvi ni kati ya Standard Chartered Bank anayodai yeye ni mmiliki wa IPTL na PAP ambaye sasa kwa sasa ndiyo mmiliki halali wa IPTL kwa mujibu wa sheria za nchi. Mpaka hapo hukumu nyingine ya Mahakama itakapotolewa na kuthibitisha vingine ama kufuta hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania iliyotolewa na Jaji Utamwa, PAP itaendelea kuwa mmiliki halali wa IPTL.

Naomba hisani yako unieleze kwa kifupi sasa nini chanzo cha ugomvi wa mabepari hawa wawili kwa uelewa wako. Kwa maneno mafupi tofauti na yale uliyoyaandika. Naamini hii itatupa faida na kutufunulia wengi chanzo cha tatizo.

Naomba ujue tofauti ya HOJA na MAONI. Kusema tu mimi nafikiri wewe ni muongo bila ya kutoa vielelezo na ushahidi uliokupelekea kufikia hitimisho hilo, hiyo inabadi kuwa maoni yako. Lakini pindi utakapoanza kutoa vielelezo na ushahidi then inakuwa hoja yenye haki ya kujadiliwa.

Hivi kipindi kile kuhusu hati ya kuitwa Mahakani Zitto niliposema wewe muongo na kuthibitisha na hata wengine kukusaidia kuthibitisha kisheria hivi ulikubali kama uliongopa? Hebu nikumbushe!

Asante
 
Hivi hujui kama ripot za PAC zilikuwa mbili? Moja iliandaliwa na serikali hiyo ilikuwa batili na iliyotukuka inawapelekesha hadi leo.
Acha uongo, hakuna Ripoti BATILI kama unavyodai. Ripoti ya PAC iliiitwa "TAARIFA YA KAMATI KUFUATIA MATOKEO YA UKAGUZI MAALUM WA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI KATIKA AKAUNTI YA TEGETA ESCROW ILIYOKUWA KATIKA BENKI KUU YA TANZANIA"

Huo UBATILI unaoudai wewe uko wapi?
 
Kwa hiyo tibaijuka tra wanamuonea?
 
Ni nini chanzo cha kukwama pesa za mcc? Ina maana nao wazungu walikurupuka? Kwa nn walisisitiza pesa zao zingetoka hadi maazimio ya escrow ya kuwawajibisha wezi yafanyike? Na je ina maana zitto alishawishi had kamat ya mcc kuzuia zile pesa kwa kuwa katunga huo uongo?
Usichanganye mambo. Fedha za MCC zilizuiwa kutokana na uchafuzi wa uchaguzi wa Zanzibar. It has nothing to do with Escrow.
Misaada iliyozuiwa na baadaye kuruhusiwa baada ya MCC ni ile ya Waingereza na nchi wahisani wengine ambao walishawishiwa na ubalozi wa Uingereza. Ubalozi wa Uingereza una mkono kwenye suala hili. Rejea mjadala mkuu wa uzi huu utaelewa.
 
Acha utoto wako kumbe hufai unaongopa mchana kweupe saada mkuya alikuwa anabishana bungeni na kafulila uchaguz wa awamu ya magufuli ulikuwepo?
 
Usichanganye mambo. Fedha za MCC zilizuiwa kutokana na uchafuzi wa uchaguzi wa Zanzibar. It has nothing to do with Escrow.
Misaada iliyozuiwa na baadaye kuruhusiwa baada ya MCC ni ile ya Waingereza na nchi wahisani wengine ambao walishawishiwa na ubalozi wa Uingereza. Ubalozi wa Uingereza una mkono kwenye suala hili. Rejea mjadala mkuu wa uzi huu utaelewa.

Pesa za mcc zimekutana na matukio mawili makubwa wizi wa tegeta escrow na uchaguzi wa zenji ukiwa muongo usiwe mwepes wa kusahau.
 
Wewe mleta mada unatumika na nani????

Bottom line, Je tumeibiwa kama nchi au hatukuibiwa??? Tunastahili kulipwa au la???

Wanasiasa na waandishi wa nchi hii hawaaminiki..

Hakuna sehemu yoyote ya Ripoti ya CAG inayosema kuwa fedha zilizokuwa kwenye Escrow ni fedha za umma. PAC inajikanganya, mara inasema fedha za Tegeta Escrow ni fedha za umma, mara inasema huenda kwenye pesa hizo kuna fedha za umma kwa sababu kuna kodi ndani yake, na mara nyingine inadai kuwa kesi ya ICSID iliamua mshtaki (Standard Chartered Bank) na mshtakiwa (TANESCO) wakakae kukokotoa upya Capacity Charges. Tatizo hiyo kesi ya ICSID-2 ilifunguliwa na Standard Chartered Bank ambaye siyo mdau kwenye mkataba wa kuuziana umeme (Power Purchase Agreement). Kafungua kesi kwa kulazimisha. Isitoshe uamuzi wa kulipwa kwa fedha za IPTL zilifanyika kati ya Septemba na Desemba 2013. Hukumu ya kesi ya ICSID-2 ilitoka February 2014. PAC na mwenyekiti wake wanadai uamuzi wa IPTL kulipwa fedha za Escrow haikuzingatia uamuzi wa ICSID-2, yaani uamuzi uliofanyika kati ya Septemba na Desemba 2013 haukuzingatia uamuzi uliotoka Februari 2014.
 
Back
Top Bottom