realMamy
JF-Expert Member
- Apr 28, 2024
- 1,539
- 3,215
Kiukweli hata mimi huwa ninaogopa baadhi ya mambo yakinisibu, lakini huwa najipa Moyo kuwa yatapita tu.
Hata Liwe Jambo kubwa kiasi gani najipa moyo mwenyewe tu kuwa nitatoboa tu.
Na mara nyingi nikiwa na Changamoto huwa natumia muda wangu kubuni buni vitu vipya, kufanya kazi, kujitoa kidogo yani ili mradi nisiliwaze lile Jambo.
Na mara nyingi nikiwa katika hali hiyo changamoto yangu huwa inatatulika. Nikiwa na changamoto sipendi kabisa kujifungia ndani.
Woga ukiuendekeza unaweza acha kazi, masomo,mke na hata unaweza kujiua wakati mwingine.
Lakini mara nyingi huwa ni kitu cha kupita kama upepo.
Usikae na kitu moyoni, usiwaze sana. Jipende.
Kuwa Daktari wa Maisha yako wewe mwenyewe.