Je,ushahidi wa kimazingira una nafasi gani katika sakata hili?

The GT

JF-Expert Member
Apr 15, 2015
461
529
Umofia kwenu wakuu.
Hapa karibuni kibanda changu cha biashara kilivamiwa mara mbili katika nyakati tofauti na kufanikiwa kuiba kiasi fulani cha bidhaa.Katika kutafuta wahalifu uliitishwa mkutano wa kitongoji ambapo katika mkutano huo ilipendekezwa kuwa wenye vibanda vya biashara katika kitongoji hicho wapatao 17 wapige kura za kutokuwa na imani ambapo matokeo yalionesha kuwa my workmate(kiajira tena ni mzawa wa hapahapa kijijini) alipata kura 7,kura 6 zilisema sijui na kura 4 waligawana wanavijiji wengine.
Hivyo nikitumia vielelezo vifuatavyo:-
1.Kura 7 alizopata workmate wangu za kutokuwa na imani.
2.Huyo workmate kutohudhuria mkutano wa kitongoji ulioitishwa na m/kiti kijiji ambao ulituhitaji watumishi wote kuhudhuria na wenzake wote walihudhuria ishpokuwa yeye wakati taarifa alikuwa nayo.
3."Kuku wa jirani aibiwe mimi nikose usingizi" ni kauli aliyoitoa kwa staff member mwingine alipoulizwa kwanini hakuhudhuria mkutano.
Je,kwa mazingira hayo huyu hahusiki kweli? je,nikimshitaki vp nitaipata haki yangu?
 
Hadi hapo hakuna ushahidi au kielelezo chochote cha kukuwezesha kumshtaki mahakamani na hatimae mahakama kumtia hatiani.
 
Labda kama utaamua kumnambikizia kesi nyingine lakini sio hii.
 
Nashukuru kwa ushauri wenu wakuu.Nathamini uwepo uwepo wenu.
 
Na kwa nyongeza ni kwamba kuna sakata linalofanana na hili lakini alihujumu mali za taasisi kwa kuiba lakini mwisho wake ushahidi wa mazingira kama hivihivi ulitumika kumtia hatiani kwani hoja zote za kimazingira zilizowasilishwa na walalamikaji hakuzikana ila alikuwa anapiga chenga kwa kuwanawia watu wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…