Je, unawafahamu hawa kwa sura?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,715
729,882
Nawazungumzia Mungu mkuu (sio miungu) shetani na malaika... Katika mkondo huo pia kuna mapepo majini mizimu nk

Neno linasema..... Basi natuumbe mtu kwa mfano wetu.... Kwa mujibu wa maandiko matakatifu haya yalikuwa ni maneno ya Mungu mkuu...
Tafsiri yake ni nini?
Kwamba kulikuwa na maisha kabla ya uumbaji wa dunia na mwanadamu... Na ya kwamba Mungu hakuwa pekeyake..... Most likely alikuwa na malaika ambao walikuwa Wasaidizi wake..... Lakini ndani ya huyu Mungu mkuu alikuwepo Mungu baba(The source chanzo asili) Mungu mwana (physical body mwili uharibikao ) Mungu roho (conscious body roho isiyokufa ) ...dhana ya utatu mtakatifu.... Mimi nipo ambaye nilikuwepo nipo na nitakuwepo (milele) yeye nani? Mungu mkuu katika utatu wake.....


Kwa ufafanuzi huo sisi ni mfano wa Mungu kwa umbo,(asili) ni mfano wa Mungu(kwa mwili wa nyama) ni mfano wa Mungu (kwa pumzi ya uzima)
Tuliumbwa tukiwa masanamu yasiyo na uhai mpaka pale tulipopuliziwa pumzi ya uhai...
Baada ya hapo Siri ya uumbaji imebaki kwake yeye kupitia uzazi.... Uumbaji mwingine wowote umeshindwa kabisa kufikia viwango vya Mungu mwenye enzi yote
Ni katika kujaribu kuumba kama Mungu tumejikuta tunaumba, tunachonga, tunachora na kutengeneza masanamu na mapicha huku mengine tukiyaabudu na kuyaogopa kabisa
Kwa fikra za kawaida za kibinadamu na mtazamo juu ya kile alichomaanisha Mungu tumejikuta tunajichorea na kujitengenezea mipicha ya kutisha kufurahisha kufariji na hata kuchekesha kabisa
Hatumjui Mungu kwa hakika wala shetani wala malaika, picha zote tunazoziona ni kwa muktadha na mtazamo wa kibinadamu kutokana na maandiko
Kwamba shetani na kaliba yake ni madude mabaya ya kutisha sana...
Kwamba malaika ni viumbe wapole wenye mvuto sura nzuri mavazi meupe ya kupendeza sana nk
Tulichonyimwa ni ufahamu wa kiroho ufahamu wa Kimungu ambao kama tukiufahamu wote basi tutakuwa tumeifikia ile njia ya ukamilifu wa Kimungu
Usitishike wala kufurahishwa na mapicha ya wanadamu.... Hayana uhalisia... Viumbe roho havina umbo wala sura maalum
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…