Je, unafahamu kuwa una wajibu wa kuzipisha daladala (mabasi ya umma)

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
15,583
23,399
JE, UNAFAHAMU KUWA UNA WAJIBU WA KUZIPISHA DALADALA (MABASI YA UMMA) ZITOKE KWANZA KITUONI KABLA WEWE ULIYEPO NJIA KUU HUJAENDELEA NA SAFARI?

NDIYO, ni sheria ipo. Kwamba ili kurahisisha mwenendo wa magari ya umma yanayobeba abiria maeneo ya makazi, dereva wa gari nyingine yoyote analazimishwa kupunguza mwendo na ikiwezekana kusimama kabisa ili kulipa kipaumbele gari la abiria liondoke kwenye kituo cha basi lilipokuwa limesimama kushusha au kupakia. Sasa sio daladala linataka kuondoka kituoni wee unalibania. Ujue utakuwa unatenda kosa na ukikamatwa utaadhibiwa kwa mujibu wa kifungu cha 54 (1)2,3 cha Sheria ya Usalama Barabarani.

Wengi wetu huwa hatuwapishi au kuwaruhusu daladala waingie barabarani kutoka vituoni, na ndio mojawapo ya sababu madereva wengi wa daladala huwa wanashushia barabarani kwenye lane (ambalo ni kosa) kuogopa wakiingia vituoni watabaniwa kutoka. SASA ndio ufahamu daladala ana kipaumbele (priority) ya kutoka na kuendelea na safari kuliko wewe mwenye gari jingine.

Ni imani yangu sasa utawapisha daladala au mabasi makubwa ya mikoani yanayotaka kushusha abiria vituoni yaingie barabarani kwanza.
 
Unapotoa elimu na kuweka kifungu cha sheria, ni vizuri ungekinukuu ili tujue kinasemaje.
 
Kwa Dar naamini hata trafiki hawaijui hio sheria maana tungekoma
 
kama ya kwenye mwendokasi pekeyake wanaingia na kuendesha migari ya polisi na kila mtu anapita humo kwenye njia maalum za mabasi unategemea daladala la kawaida lipishwe na magari mengine?
 
Back
Top Bottom