Kukufuru ni kujiweka ktk nafasi ya Mungu ingawa wewe ni mwanadamu Yohana 10:33 Wayahudi wakamjibu, kwa ajiri ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe ulie mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu. ---->hiyo ndo maana ya kukufuru. Kudai kuwa sawa na Mungu.
==>Isaya 14:13,14 Shetani alitamani kupaa juu kupita nyota za mbinguni ili afanane na Mungu, yaani akakae ktk nafasi ya Mungu.
==>Mwanzo Mwanzo 3:5 Shetani aliuingiza ulimwengu dhambini kwa kosa la kufuru yaani alimshawishi Eva akaidi agizo la Mungu amwahidi kuwa "atakuwa kama Mungu"-->hii ni kufuru!
WAKATOLIKI wana mwanadamu waliempa jina lenye wadhifa na wasifu wa Mungu peke yake, yaani " Baba Mtakatifu" Soma: Yohana 17:11Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba Mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.
Umeona hiyo aya inavobainisha kuwa "Baba Mtakatifu" ni jina la Mungu? Lakini Wakatoliki wana babao mtakatifu mwingine!!!!!? KUFURU!.
Mathayo 23:9 Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni. 10. Wala msiitwe viongozi; maana kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo.
Ndugu zangu aya hii ya 9, Mungu kakataa kuwa na ubia ktk jina lake la mamlaka linalobeba wadhifa wake. Kumwita mtu baba Mtakatifu na kiongozi mkuu wa dini ni KUFURU.
Mwenye masikio na asikie ambayo roho awaambia Wakatoliki. Mimi ni mjumbe tu kuwakumbusha yaliyokwisha bainishwa