Nifahamuvyo mimi nafsi inahusisha; haiba, elimu, ujuzi, tabia, hekima, weledi na mambo kama hayo! Katoto kanavyozaliwa kana mwili, roho na nafsi ambayo mara nyingi ni "emotions" na "instincts"! Sasa sisi wazazi tunaiendelza nafsi yake kwa kumpa maarifa mbalimbali yamkini mengine ni ya kudhibiti emotions na instincts zake hususani zilizo na matokeo hasi! Baadae huwa mtu mzima na kuiendeleza nafsi yake zaiidi! Kwa uelewa wangu huu nafsi ya mtu hubaki kumbukumbu duniani kutokana na kazi aloziacha! Ukatili, udikteta, uasi, utu, wema, mchapisho, majengo, sanaa, hila n.k. ni madhihirsho au matendo ya nafsi (rejea ee nafsi yangu mhimidi bwana)! Kwangu mimi nafsi ndiyo inayoidhibiti roho na mwili ili kupata matokeo mema! Nafsi inaweza kuikaribisha roho wa Mungu au Shetani! Kazalika nafsi ndiyo inayoyadhibiti matendo ya mwili! Mwili hudhihirisha nafsi ya mtu na yaliyomo rohoni mwake!