Je, Meya Dar es Salaam anazindua kundi la kufanya vurugu (chawa)? Matumizi ya chawa ni njia mpya ya kuvuruga mikutano ya upinzani

seedfarm

JF-Expert Member
Feb 9, 2020
260
2,655
Uzinduzi wa vijana wa vurugu au kwa jina la kisasa chawa watakaotumika kuwavaa watu wa upinzani hautaishia Dar es Salaam pekee,

Meya wa jiji la Dar es Salaam anatumika kama chambo tu kuzindua anachokiita"Chawa wa Mama", CCM hawajapima Madhara ya uzinduzi huu

Uzinduzi huu wa Machawa utasababisha kila chama kuwa na genge lake la kufanya fujo na vurugu nchi nzima kwenye mikutano ya siasa

Rais Samia alishasema chawa wake wanaweza kuwavaa wanasiasa wa upinzani pale watakapo toa kauli kinyume na matarajio yao

Matarajio ya vijana hawa wa ccm waitwao chawa ni kuharibu mikutano ya upinzani kwa kufanya fujo na vurugu pale jina la Rais litakapotajwa

CCM kama CCM walishindwa kujibu hoja za Tundu Lissu bungeni kuanzia hoja za muungano, Hoja za mikataba ya madini (Hapa ccm waliahidi gari za Noah kwa kila mtanzania aliyezaliwa na aliye tumboni) Mwisho wa siku yalitokea ya kutokea kwa Tundu Lissu, Baada ya JPM kufariki akina Kabudi profesa na genge lake wanasema hatukuwa tunawadai Acacia bali zilikuwa mbinu za majadiliano ili kumlaghai Rais na kum pet peti kwa uwongo

Kwa miaka zaidi ya sita ccm walikuwa wakiwadanganya wananchi peke yao, Muda wa kujibu ule uwongo wa miaka sita wa kwenda Birngham City kwa vijana wa Kawe unaogopwa sana na sasa tegemeo la ccm ni chawa(Vijana wa fanya fujo na vurugu)

Hoja ya bei za vyakula, CCM Wamepewa muda wa kujibu kwa mwaka mzima wameshindwa, Wamezunguka Tanzania yote, Wamefanya mikutano wao tu nchi yote bei za vyakula zinazidi kupanda, Sasa wanategemea chawa wawasaidie kufanya fujo na vurugu wapinzani watakapo ongea majukwaani kuhusu hali ya mfumuko wa bei.

Ni muda wa serikali kukemea aina hii ya vijana wanaojiita chawa kwa minajiri ya kuwa brain washed kwa kujazwa itikadi za kuwa mtu wao hapaswi kusemwa hovyo au kuambiwa ukweli

Hali hii ya viongozi kutotakwa kusemwa( mwaka 2015 mpaka Mwanzoni mwa mwaka 2021) na kujiona wao ndio kila kitu yaani alfa na omega ilisababisha wananchi kuanza kuombea vifo viongozi wao na hata pale kifo kilipotokea baadhi ya makundi yalifanya sherehe ya kukata na shoka

Endeleeni kuzindua "Machawa". Time is loading...

We see dangers threatening our peace kisa tu chawa
 
Endeleeni kuzindua "Machawa". Time is loading...................

We see dangers threatening our peace kisa tu chawa
Hawa CHAWA sasa imekuwa ni jumuia mpya ya chama tawala.
Screenshot_20230105-083929.jpg
 
Mbona unaanzisha maada usiku wa manane watu wakiwa wamelala???
Wewe ni mchawi au unaogopa wakiwa macho??
 
Kutojitambua uwepo wa mtu duniani na kusudio la kuwepo, ujinga, umasikini wa mali na akili, kujipendekeza, uchu wa madaraka, kuficha maovu, ushabiki wa bila maono, chuki dhidi ya wasema ukweli, kutopenda kujifunza mapya, kulaghaiwa kama changudoa gizani, kupenda wepesi wa maisha, kujionesha pasina tija na uhayawani ni vyanzo vikuu vya kuijinasibisha na uchawa.

Na ndiyo maana huchekelea waitwapo ng'ombe waliokatwa mikia, mang'ombe au majina yote mabaya. Ni ulegevu na upotofu wa hekima na utashi tegemewa wa kibinadamu.
 
WANATAFUTA NAMNA YA KUPIGA HELA TU,NDOMANA UKIWAANGALIA WOTE MATUMBO YAO MAKUBWAAA

ova
 
Hii Nchi.

Yaani toke Shaka abebwe kwa Warabu na kuka meza kuu na wafadhili, Jeuri zao zimekuwa Maradufu.
Wakati wao wanaweka Pesa, Fedha, Hela kwenye sinia kwa aajili ya "Official Chawa" Basi ni muhim Wananchi kufikiria kile ambacho kitaondoa karaha za Chawa, kwa kuweka Kura kwenye Boksi 2025. Sasa huko, waje wawavae kama hawatavuliwa! Mumohumo, kwa Boksi.
 
Back
Top Bottom