Je, kwa maneno haya ya Mzee Butiku nae hatotembelewa kwa 'Kushtukizwa' Kwake Mabwepande kama akina Msuya na Warioba?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,214
"Vijana lazima wajue kuwa Chaguzi za Siku hizi nchini ni za hovyo na zimejaa Rushwa, Fujo na hakuna Haki halafu Viongozi hawapendi Kukosolewa na Wananchi ili wajitathmini na wabadilike. Suala la Katiba Mpya huenda likawa na Mashiko kwa wale wanayoitaka sana hivyo wasikilizwe"

Chanzo: Radio One Promo yao ya Kipindi cha dakika 45 cha Kesho Jumatatu ( tarehe 6 Disemba, 2021 ) kuanzia Saa 3 Kamili za Usiku ITV na Radio One.

Wazee ( Mawaziri Wakuu Wastaafu ) akina Warioba na Msuya kwa nyakati tofauti Mwezi wa Novemba waliongelea Suala la Katiba, Demokrasia na Ufisadi Wiki hii wakatembelewa 'Makwao' hivyo kuna uwezekano hata Mzee Butiku ( Msaidizi na uliokuwa Ubongo wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ), Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Kada Mwandamizi wa CCM akatembelewa Nyumbani Kwake Mabwepande.
 
Katiba mpya haina mjadala.Ukiona mtu au kikundi cha Watu kinapinga Katiba Mpya jua wanaangalia maslahi yao ya wakati huu.
 
Back
Top Bottom