Tetty
JF-Expert Member
- Jan 6, 2012
- 26,355
- 21,396
Dah tatizo tunaweka ushabiki mbele kuliko kuangalia uhalisia wa jambo lenyewe... ishu hapa siyo mbunge aliyetukana kuchukuliwa hatua ama la... kwanza hajulikani hata ni nani... hata Mnyika mwenyewe hamjui ni nani.. na Spika nae hamkujua ni nani. Tunachokiongelea hapa ni suala la Mnyika kudharau Mamlaka ya Spika period.. jambo ambalo ni kinyume na kanuni za Bunge
SIoni kama alimdharau Spika ni namna tu ambavyo hukumu ipo upande mmoja,ilipotolewa adhabu kwa Halima walikuwa wengi wakizomea na kutukana aliyesikika alikuwa Halima,tuache ushabiki wa uvyama,Spika angeweza tu kumuelekeza Mnyika ku-cool down wakati anaishughulikia issue yake,kwanza alitakiwa kumsikiliza na siyo kumlazimisha kutoka nje.Angemtuliza na kumsikiliza,huo ndiyo uongozi,lakini si kukurupuka na kuwatoa nje,aliyetukana amefanywa nini??
Je baada ya kutoka ulimsikia Spika akijisifu na kuweka msisitizo namna atakavyo wakomesha na kuilazimisha Kamati ya MAADILI kuwapa adhabu,na kwanini aseme sitaki kukuona BUNGENI hivi BUNGE ni la SPIKA??
SIpendi namna ambavyo bunge linaendeshwa,tulidhani jinsi miaka inavyoenda Viongozi wabunge watajifunza kuwa wavumilivu kumbe UKADA,WIZI na ujangili ndivyo vimewajaa.
Niliona sakata zima lilikuwa limepangwa ili Bajati ya WIZARA husika ipite bila tatizo,ukiniambia hivyo naweza kuelewa.
Lusinde anatukana sana wabunge wa upinzani,uliwahi kusikia anatolewa nje au kutumikia kifungo??AU kupelekwa kamati ya maadili??Mbunge yupi aliwahi kupelekwa kamati ya maadili??Kwanza hiyo kamati yenye wajumbe 90% CCM ndiyo inayotoa hukumu??Kesi ya nyani unaipeleka kwa ngedere.