Majini ni malaika walio muasi Mungu pamoja na Shetani ,Majini yanatumiwa na shetani kutumikisha watu. wakrito wanayaita mapepo .Hakuna ushirika wowote kati ya ukristo na majini au mapepo ,kiufupi hayataki jina la Yesu. Ila kuna ushirika mkubwa kati ya uislamu na Majini, wanaswali nayo wanasema ni maislamu .Mimi hapo ndio napata mashaka makubwa juu ya Dini hii.
Kwa bahati mbaya sana mambo yahusuyo majini katika imani ya Kiislamu ni tofauti sana na vile tulivyosoma katika Biblia. Ingawa Quran na Hadithi za Muhammed, Mtume wa Waislamu, Vinatutaka sisi wakristo tumwamini allah S.W. mungu anayeabudiwa na Waislamu Misitikini.
Katika Suratul Waqia 51:56.
“Sikuwaumba majini na watu ila wapate kuniabudu” katika Quran Suratul Al- Ankabut (Buibui), 29:46-47) “ Wala msibishane na watu waliopewa kitabu (kabla yenu) ila kwa yale (majadiliano) yaliyo mazuri isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao na semeni tunaamini yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwenu na Mungu wetu na Mungu wenu ni mmoja nasi ni wenye kunyenyekea kwake”.
Waliopewa kitabu kwa mujibu wa Quran ni Wayahudi na Wakristo. Je, hoja kuwa Mungu wetu na Mungu wao wanayemwabudu kuwa ni mmoja je ni sahihi?. Tuchunguze kuhusiana na mafundisho ya Allah S.W. wa misikitini kuhusu majini ndipo tutajua ni mmoja au la!
Muislam yeyote ili imani yake ikamilike ni lazima aamini yanayoonekana na yasiyoonekana katika Suratul Al- Baqarah (Ng’ombe Jike la Njano), 2:1-3.
“ Alif Lam Mym. Hiki ni kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake ni uongozi kwa wamchao mwenyezi Mungu ambao huyaamini yasiyoonekana (maadaam) yamesemwa na mwenyezi Mungu na Mtume wake) husimamisha sala na hutoa katika yale tuliyowapa.
Quran peke yake ukiichunguza utaona kuwa majini yamechukuliwa kama ni viumbe tofauti na mashetani, wanasema hivyo kwa sababu katika uislamu majini yamepewa hadhi kubwa sana na ya kipekee. Hadhi hiyo ni kwa sababu majini waliamini Quran.
Tusomapo katika Quran Suratul al- Ahqaf, (Kichuguu cha mchanga) 46:29
“ Na (wakumbushe) tulipokuletea kundi la majini (kuja kwako) kusikiliza Quran. Basi walipoihudhuria walisema (kuambiana):- “ Nyamazeni (msikilizeni maneno ya Mwenyezi Mungu)” Na ilipokwisha (Somwa) walirudi kwa jamaa zao wakiwaonya”.
Na ndani ya Quran kuna sura nzima inayoitwa sura ya majini (Mashetani) hiyo ni sura ya 72. katika sura hiyo inasema 72:1-3, 14. “ Sema: imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la majini liliisikia (Qurani) likasema hakika tumesikia Qurani ya ajabu inaongoza katika uongofu. Kwa hivyo tumeiamini wala hatutamshirikisha yoyote tena na Mola wetu na kwa hakika utukufu wa Mola wetu umetukuka kabisa. Hakujifanyia mke wala mwana…. Nasi wamo miongoni mwetu na wamo miongoni mwetu waliokengeuka waliosilimu hao ndiyo waliotafuta uwongofu.
Kwa hiyo aya hizi zinaonyesha kuwa Quran ilipokuja ndipo majini waliposilimu. Kumbuka kuwa Quran imeanza mwaka 610 B.K kipindi ambacho Biblia tayari ili kuwepo kwa karibu karne 6.
Akifafanua asili ya majini Mwanazuoni mkubwa wa kiislamu aitwaye Abdalllah Saleh Farsy aliye kuwa Kadhi Mkuu Zanzibar, kisha akawa Kadhi Mkuu Kenya katika kitabu alichoandika kiitwacho “Maisha ya Nabii Mohammad” ule Uk. 31 anasema “ Katika safari yake ya kurejea Taif ndipo walipomjia majini wakasilimu kama inavyoonesha haya katika Suratul Jinn. Majini ni viumbe vyepesi vinavyokaa angani. havina viwiliwili kwa hiyo haviwezi kuonekana na wanadamu ila vinapojibadili kwa umbo lenye kiwiliwili. Na vina uwezo huo wa kujibadili kwa sura ya kuweza kuonekana. WAO NA MASHETANI WANA ASILI MOJA. Kwa hiyo asili ya majini ni shetani.
Suala linalohusu malaika linawasumbua sana waislam hata hawana uhakika wake.
Tumesoma ndani ya Biblia kuwa kuna kundi la malaika waliokosa ambao ndiyo wanaoitwa majini lakini tusomapo Quran inatoa maelezo tofauti.
Quran suratul As- Sajdah, (kusujudu) , 32:13 “ Na tungelitaka tungempa kila mtu uwongofu wake (kwa lazima kama tulivyowapa malaika lakini binadamu amepewa huria ya kufanya alitakalo- lililo jema na baya).
Katika ulimwengu wa Kiislamu Malaika wote ni8 wema na wanamwabudu mungu.
Hapa ndiyo tatizo linapoanzia. Quran iliyokuja baadaye inasema malaika wote ni wema wakati biblia kitalu kilichoitangulia Quran kinasema kuna malaika walioasi na wakafukuzwa katika utukufu wa Mungu.
Katika Quran Suratul, al- Kahf, (Pango) 18:50 “ Na (Kumbukeni) tulipowaambia Malaika, Msujudieni Adamu. Basi wakamsujudia isipokuwa Ibilisi yeye alikuwa miongoni mwa majini na akavunja amri ya mola wake……..”
Katika aya hiyo tunaona ibilisi akilaumiwa kwa kutomsujudia Adamu ingawa amri ya kusujudu walipewa malaika kumbe kwa mujibu wa Quran Ibilisi alikuwa miongoni mwao hao malaika yaani na yeye akiwa malaika.
Kwa sababu Quran haina habari kuhusu malaika walioasi yaani majini ndiyo maana wanapata tabu kuhusu jambo hilo. Na ndiyo maana pamoja na kujua kuwa hayo majini ni mashetani, Muilsamu amehiari kushirikiana nayo kwa kuswali nayo msikitini. Na hata mwislamu huyu anapomaliza kusali husalimia kulia na kushoto akiwasalimia watu malaika na majini (mashetani) waliokuja kushiriki naye katika Ibada yake, soma katika (Irshadul Muslimiin, Sheikh Said Musa, Uk. 38).
Katika Tafsiri ya Quran ya Iman Jalalaini Uk. 6:151 anasema kuhusu majini “ Hao ni watoto wa Ibilisi”.
Hii ndiyo sababu hata wanawake wa Kiislamu wakiwa katika kipindi cha hedhi hawaendi msikitini kwa sababu kuna majini na chakula cha majini ni damu. Tafakari kwa hiyo sifa ya hayo majini au mashetani kwa ujumla ni kuwa “ hujaribu kwa bidii sana kuwa karibu na waamini wale wanaosali, kufunga na kusoma Qurani “ (Asili ya majini, Dk. Ahmed H. Sakr Uk. 28) ndiyo maana baadhi ya waislam wao binafsi wasingependa kuwa waislamu lakini majini huwashurutisha kwenda kuswali.
Kwa sababu wao waislamu hawajui kupambanua kati ya majini ambayo ni roho chafu na wale malaika watakatifu wa Mungu Jehova, ndiyo maana hata akiwa katika sala yake hana uhakika kwa sababu huyo jinni (shetani) amemteka na anamfanyia atakavyo na yeye ni mtumwa wa huyo jinni (shetani).
Katika kitabu kiitwacho Mkweli Mwaminifu cha Sheikh Said Moosa Mohamed Al- Kindy wa Muscut Oman, juzuu 1-2 Uk 42 Hadithi Na. 74.
“ Anamwijia mmoja wenu shetani (Jini) katika sala basi anapuliza (anampuliza) katika matako yake, basi (yule mtu) inamuijia fikra ya kuwa umemtoka upepo (kafusa) naye haukumtoka, basi akiona namna hiyo asiondoke (kwenye sala}) mpaka asikie sauti ( ya kutoka upepo) au anuse harufu ( ya huo upepo uliyomtoka, ndio aondoke).
Katika kitabu kiitwacho Asili ya Majini, cha Sheikh Dr Ahmad H. Sakr Uk. 116 anasema “ Hadithi ya Mtume inathibitisha jambo hili kuwa majini (mashetani) na watu wanaweza kuoana aliposema kwamba iwapo mtu ataingia katika uhusiano wa kindoa na mkewe anatakiwa ataje jina la Mwenyezi Mungu ajilinde kwa Mwenyezi Mungu dhidi ya shetani aliyefukuzwa mbali na rehema. Vinginevyo shetani hujiviringisha katika dhakari (sehemu ya siri za mwanaume) ya mtu huyo na atashirikiana naye katika tendo hilo.
Tafakari yetu kuwa hiyo jinni anayeshiriki naye tendo la ndoa pamoja naye kwa mkewe ametumwa na nani?