Janga jipya: Zanzibar yaishiwa Mchanga, sasa kuagizwa nje ya nchi

mchanga unaotoka same kenda moshi 150000 kuendelea!


Mkuu;
Si ndo maajab hayo?? Wao ati laki wanalia. Sasa wanategemea huo wa kuagiza ng'ambo uwe elf themanini au?? Semeni bei tuwaletee kwa mafuso, wengine hatuogopi bahari ila rupia yangu muiweke bank kwanza
 
Kusema kuna upungufu wa mchanga inaruhusiwa ila kutangaza upungufu wa chakul* ni jinai
 
Lori la mchanga laki moja,? Mbona huku dar lori ni laki mbili unusu?
 
Wawe makini na uchimbaji mchanga... Wasije wakaitoboa zanzibar alafu ije kuzama...
 
Nimeshangazwa kuadimika kwa mchanga huko Zanzibar, haya ni maajabu. Ni laana au? Hivi wengine wanalalamika kuadimika kwa mvua, chakula, sukari, mwenyewe udongo. Haya majanga mie nadhani ni........ Kha nchi yetu haiishi vituko.
chukua fursa acha kulalamika kama mtoto,peleka mchanga zanzibar,kodi jahazi mwaga lori zako mbili nenda kauze,unakaa unashinda humu kazi kulaumu na kulalamika tu,ushafika zanzibar wewe?mji wote unajengwa ma apartment na mahoteli,kisiwa chenyewe ukipiga filimbi mtu alieko shamba anakusikia
 
Pole yao, wabuni na waige njiannyengine za ujenzi wa nyumba zisizohitajichanga mwingi kama za mbao.

Nimeona fumba kwenye mji wa kisasa wa mzee Bakhressa kuna nyumba za kijerumani anajenga za mbao, ni nzuri zinadumu na nafuu
 
Mchanga Huo Ni Huu Unaopatikana Popote
Nimejaribu Kujiuliza Maswali Kama Ngumu Kuamini ? Tanganyika Ipo Hapo Halafu Wakaagize Sijui Ughaibuni

Mbona Bara Michanga Chekwaa Hata Pamoja Na Mfano Hivi Viwanda Vya Saruji Mfano:-
Simba Cement Tanga
Tembo Cement Mbeya
Twiga Cement Dar
Hapo Nimetaja Vile Vikongwe
Hivi Vipya Navyo
Rhino, Mkombozi,Camel,
Sijasikia Uhaba Hata Wa Limestone Sembuse Huo Mchanga
 
Mi nimemshangaa mwandishi wa ITV kusema mchanga ni nishati.
Wanaojua watujuze mchanga uko kwny form ipi ya nishati!!
 
Nadhani swala la mvua kutonyesha kwa kiwango cha kutosha pia linachangia.
 
Hamad Rashid ametangazia dunia kwamba Nchi ya Zanzibar imeishiwa mchanga kwaajili ya Ujenzi, hivyo wameruhusu kuagiza mchanga toka nje bila kodi.
View attachment 465256
Serikali ya Zanzibar imeomba wadau wajitokeze kuagiza mchanga nje ya nchi ili ujenzi uweze kuendelea.

Kwa sasa lori la mchanga linauzwa kwa laki moja na na bado haupatikani kwani kila sehemu walipokuwa wanachimba umeisha.

========

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema imekusudia kuagiza mchanga nje ya nchi kutokana na kupungua kwa kiasi kikubwa kwa rasilimali hiyo hapa nchini.
View attachment 465030
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Waziri wa kilimo Maliasili Mifugo na uvuvi Hamad Rashid amesema Zanzibar haina mchanga utakaokidhi mahitaji ya ujenzi kutokana na kiwango kikubwa cha rasilimali mchanga kuchimbwa kwa kasi unguja na pemba.

Hata hivyo amesema ili kupunguza tatizo hilo lazima serikali kutumia matumizi mbadala wa mchanga katika harakati za ujenzi au mbinu za kutumia mchanga kidogo na kubuni rasilimali nyengine badala ya mchanga ili kupunguza tatizo ambalo linaathiri hapa nchini.

Aidha amesema hali imekuwa mbaya kutokana na matumizi mabaya ya ardhi inayosababisha athari kuongezeka hivyo serikali inatumia hatua za dharura kudhibiti uchimbwaji wa mchanga lazima utaratibu wa utoaji vibali ubadilike kutokana na upungufu uliopo ili kudhibiti rasilimali chache ilobaki.

Ametoa wito kwa wananchi kuwacha kuchimba mchanga kiholela na wanaochimba katika maeneo ya kuvunia kuwachana na serikali itatenga maeneo mbadala yatakayo tumika kwa shughuli hizo na kwa utaratibu maalum.

Utafiti uliofanywa hivi karibuni kwa Unguja na Pemba imeonesha kuwa Unguja inachimba hekta 3 kila mwezi na Pemba nusu hekta kila mwezi ambapo kwa mwaka 2016 uchimbaji huo umefikia tani Million moja laki nane na arobaini na sita elfu.

Credit: Amina Omar mwanahabari wa Zanzibar
ningelikuwa rais, hawa jamaa wangeniamkia shikamoo, wangenikoma. kwasababu kwanza kabisa bara imefanya mengi kwaajili yao lakini hawana shukrani, ardhi wakiwa huku wanaruhusiwa kumiliki hata ekari milioni lakini sisi tukienda kwao hawaturuhusu kumili na ukibahatika, utauza we mwenyewe bila hata kuambiwa na mtu uuze kwa jinsi watakavyokushughulikia, na utakayemwuzia ni mzenji. kanchi kao kamejaa udini wa hali ya juu, siku za mfungo wakristo hawaruhusiwi kuuza chakula mchana wakati wao hawafungi, wameshalipua kwa mabom ya petrol makanisa mengi sana na wanalifurahia hilo, serikali haina uwezo kuzuia hilo au sijui inalispaoti hilo huwa sielewi. pamoja na kujifanya waswahilina kiasi hicho, ndio sehemu yenye ushoga kuliko sehemu zote tz, utalii wa wazungu unategemea wazungu mashoga na wanaowaita makafiri. huwa nashangaa sasa kuswali kwao si kuwasaidie watakate mwili na tabia ili uchafu huo usitajwe kabisa zenji, lakini hadi leo ukienda zanzibar na mombasa, Tanga, ushoga au kuingilia wanawake kinyume na maumbile ni kitu cha kawaida kwao. wakiwa nje wanajifanya wanachukia, lakini kwa kuangalia mitabia ya watu walivyo inaonyesha wakiwa mafichoni wanafanya uchafu kuzidi hata ule uliofanywa na sodoma na gomora.
 
pia kisiwa chao nasikia kinapungua kila mwaka maji yanasogea, itafika kipindi watalala baharini kama samaki. tutawaruhusu waje bara lakini udini na uzanzibari wauache hukohuko Nungwi.
 
Back
Top Bottom