Comred Mbwana Allyamtu
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 351
- 866
JAMUHURI YA AFRIKA YA KATI NA MAUAJI YA FEDHEHA KWA BARA LA AFRIKA
Makala yangu no 04. Juu ya ziara yangu East, Central & Great lake zone of Africa.
Na Comred Mbwana Allyamtu.
Bangui ndio makao makuu ya nchi ya Jamuhuri ya Africa ya kati wenye wakazi takribani milioni mmoja na laki saba (1.7 million) sawa na asilimia 49.99% ya wakazi wote wa nchi nzima ambao ni milioni 4.616 wakazi wa nchi nzima ya Jamuhuri ya Afrika ya kati. Nusu ya nchi ni sehemu kame ambayo ni kaskazini mwa nchi hiyo. Uchumi wa taifa hilo ni GDP 1.539 Bilion US$ inaloliweka katika kundi ya nchi ya 37 kwa uchumi Africa na 112 dunia katika orodha ya World Economy Index. Lugha ya taifa hilo ni KISANGO lakini Kifaransa ndio lugha lasmi katika maofisi na katika shuguri za kiselekari.
Barani Africa zipo nchi mbili ambazo majina yake ni utambulisho wa mahali zinapopatikana kigeographia nchi hizo ni Jamuhuri ya Afrika ya kusini inayopatikana kusini mwa bala la Africa na Jamuhuri ya Afrika ya kati inayopatikana katikati mwa bara la Afrika. Katika makala hii tutakwenda kufanya uchambuzi na upembuzi yakinifu juu ya taifa la Jamuhuri ya Africa ya kati nchi ambayo mwenyewe nimepata bahati ya kuizuru kwa ziara ya zaidi wiki mbili na nusu ( siku zipatazo 16) nikiwa katika jiji lao kuu la Bangui na kupata fursa ya kujifunza mambo kadha wa kadha. Pamoja na ziara yangu kuwa na changamoto nyingi za usafiri ili kufika katika nchii hiyo kutokana na changamoto za balabala kutoka jiji la Kisangani katika jimbo la Oriontale katika nchi ya kongo-DRC mpaka jiji la Bangui Africa ya kati kwa njia ya balabala yenye urefu wa KM 1230. Nje ya changamoto hiyo nimeweza kujifunza mambo lukuki ambayo ndio muktadha mkuu wa makala hii ya leo.
Jamuhuri ya Africa ya kati Ni nchi ambayo haifahamiki sana masikiino mwa watu kwa maana sio maalufu sana kama ilivyo zoeleka nchi zingine hapa balani Afrika na ni nadra sana mtu wa kawaida asie mfatiliaji wa mambo ya kidripomasia kuifahamu nchi hii kiulahisi na kwa kipindi kilefu imekuwa taifa lisilofahamika lakini. Mwaka 2013 ghafra kulilindima habari duniani kote juu ya kile kilichotokea katika nchi ya Jamuhuri ya Afrika ya kati yaliyopelekea vifo vya mamia ya watu na wengine wengi kuyakimbia makazi yao. Hapa ndipo sasa watu wakaanza kuijua nchi hii ya Jamuhuri ya Afrika ya kati (CAR) na kuanza kushawishika kutaka kuifahamu kinagaubaga.
Katika ziara yangu ya nchini CAR ilioanza tarehe 8/8/2016 mpaka 24/8/2016 nilipata kuizuri jiji kuu la Bangui na kujionea hali ya maisha inayoendelea katika mitaa marufu huku ikiwamo mitaa ya Omadugudu, Benefriq ville na Ousododj katika mitaa hii ndio ukaliwa na wakazi wengi wenye maisha ya kati. Nikiwa huko ikiwa ni pamoja na kujifunza maisha baada ya machafuko ya kutisha yaliyo tokea na kupelekea vifo na wakimbizi kuikimbia nchi yao. Vurugu na machafuko yaliyokuwa yakichochewa na misingi ya kidini baina ya dini mbili yani wakristo walio ongoza kikosi cha Ant-Balaka na waislam waliogoza kikundi cha Seleka. Ningependa katika makala hii tujifunze juu ya kile nilicho kiita " JAMUHURI YA AFRIKA YA KATI NA MAUAJI YA FEDHEHA KWA BARA LA AFRIKA" katika hoja hii Kuntu nivyema tukaifahamu Jamuhuri ya Africa ya kati katika nyanja za kihistoria, kiuchumi na kisiasa.
HISTORIA YA JAMUHURI YA AFRIKA YA KATI.
Kwa zaidi ya miaka 1900 (yani mwaka 170 BC) iliyopita nchi ya Afrika ya kati imekuwa na wakazi wakiishi katika ardhi hiyo walio julikana kama "WASANGO" walio kuwa wakizungumza lugha ya "Kisango" na pia sehemu nyingine ya kusini magharibi kulikuwa na jamii ya "MBILIKIMO" (WAMBUTE) waliotoka sehemu za misitu ya Kongo, huku magharibi waliishi jamii ndogo ya "WASANI" ambao asili yao ni kongo waliokuja miaka ya 300BC kufatia vita vya makabila dhidi ya uvamizi uliotokana uhamaji wa kundi kubwa la Wabantu waliokuwa wakitoka Afrika magharibi karne ya Pili (2).
Mpaka mwaka wa 500 BC walipo kuja jamii kubwa ya wabantu wakitokea Cameron na kongo-DRC. Kukapelekea mtawanyiko mkubwa wa binadamu na muingiliano wa makabila. Mpaka mwaka 1800 uvamizi wa wazungu na kupelekea kuanzishwa kwa ukoloni Afrika. Katika Nchi ya Afrika ya kati (CAR) mala baada ya mkutano wa Berln wa 1884-5 nchi hiyo ilidondoka mikononi mwa utawala wa Ufaransa na kuwa koloni lake. Ufaransa ilitawala CAR katika "mfumo wa Ufananisho"(Assimilation system) ikiwa ni pamoja na kuwekeza katika sekta ya madini kwa kuanzisha makampuni makubwa kama "Sòcíety lé diamond du Bénéfreck" iliyokuwa ikichimba Almasi katika mkoa wa Pula.
Utawala wa kikoloni aukutoa haki za kijamii kitu kilichopekekea kuzuka migogoro mara kwa mara ikiwa ni pamoja na mgomo mkubwa uliotokea mwaka 1951 Mjini Bangui uliosababishwa na ubaguzi na unyanyasaji kwa wafanyakazi wa mashilika ya Posta, makalani wa maofisi, Walimu na wafanyakazi wa kwenye makampuni ya madini wa kiafrika dhidi ya wazungu. Katika maandamano hayo Ufaransa ilitumia nguvu kubwa kuyazima na kupelekea mauaji ya watu karibu 90 na vuguvugu hili ndio lililokuwa mwanzo wa harakati za uhuru na ukombozi wa nchi hiyo.
VUGUVUGU YA UKOMBOZI NA UHURU.
Mwanzoni mwa miaka ya 1946 mara baada ya vita ya pili nchi ya Ufaransa iliathikika sana kutokana na madhala ya vita hiyo iliopelekea Ufaransa kubadili namna mbinu za utawala katika makoloni yake. Hivyo katika nchi hii mkoloni aliongeza mbinyo katika mifumo ya uchumi kitu kilichopekekea kuongeeka kwa maandamano ya mara kwa mara kilichoongeza hali ya mapambano na mageuzi katika halakati za ukombozi. Lakini wakati hayo yakiendelea huko Ubangi-Shari kulikuwa na chief aliokuwa akiongoza vuguvugu la uhuru alieitwa Bartheremy Boganda ambaye baadae aliungana na mwalimu wa chuo cha Bangui David Dacko.
Katika mapambano yaliyo kuwa katika misingi ya kikabila na kwa upande mmoja kabila la Ngbaka lilokuwa likipendelewa na wakoloni wa kifaransa, mwaka 1956 David Dacko alishaguliwa kuwa kiongozi wa kiliwakilisha jimbo la Ubangu-Shali kwanye bunge la Bangui na mwaka 1959 baada ya kifo cha mzee Bartheremy Boganda ambacho kifo hicho kilihusishwa na wakoloni kutokana na Boganda kuanza kuonekana kwenda kinyume na matakwa ya wakoloni juu ya maslahi ya makampuni ya madini ya almasi Bartheremy Boganda alikufa kwa ajali ya ndege huko kwenye milima ya M'poko akitoke mjini Younde ndipo kwa pendekezo la wafalansa wakapendekeza David Dacko kuwa Rais wa taifa hilo watakapo ikabizi uhuru mwaka 1960. Hatimaye 13/8/1960 taifa hilo lilipata uhuru na David Dacko akawa Rais wa kwanza kwa msaada wa wakoloni baada ya kumshinda mpinzani wake aliyeungwa mkono na umma bwana Abel Goumba aliye ongoza kwenye kura ndani ya bunge lauwakilishi mjini Bangui.
Hata hivyo Kwa miongo mitatu kutoka uhuru, ‘Jamhuri ya Afrika ya Kati’ ilitawaliwa na serikali za mabavu zilizonyakua mamlaka bila kufuata taratibu za demokrasia. Kwa namna ya pekee Jean-Bédel Bokassa alitawala kuanzia tarehe 31 Desemba 1965 hadi Septemba 1979, na aliingia madalakani kwa kumpindua momba wake David Dacko. akijifanya kaisari tarehe 4 Desemba1976 alipopinduliwa. Mwaka wa 1993, kura za kidemokrasia za kwanza zilifanywa na kumchagua Ange-Félix Patassé kuwa Rais. Lakini Rais Patassé alipinduliwa na Jenerali François Bozizé mwaka wa 2003. Baadaye huyo Bozize alishinda uchaguzi mnamo Mei 2005 na kuiongoza nchi mpaka Machi 2013 alipolazimika kukimbia kufatia machafuko ya kikundi cha Seleka kutaka mageuzi.
Kati ya Novemba 2012 na tarehe 23 Julai 2014 vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipamba moto nchi nzima na kuibuka mauaji ya kutisha na maerfu ya wakazi kuikimbia nchi.
KUIBUKA KWA MACHAFUKO YA KIDINI NCHINI AFRIKA YA KATI
Jamhuri ya Afrika ya Kati imekuwa katika vita vya wenyewe tangu mwezi Machi mwaka 2013 baada ya kuondolewa madarakani kwa Rais wa muda mrefu Francois Bozize kupitia mapinduzi ya serikali yaliyofanywa na waasi wa kundi la kiislamu la Seleka.Mapinduzi hayo yalichochea mashambulizi ya kulipiza kisasi na kuibuka kwa kundi la waasi la Kikiristo la Anti Balaka. Maelfu ya watu nchini humo wameuawa tangu kuzuka kwa ghasia hizo na mamilioni ya wengine wamelazimika kuyahama makaazi yao. Vita vimekuwa CAR tangu 2013 pale Waasi wa Seleka walinyakua mamlaka mwezi Machi mwaka 2013 na kumuidhinisha Michel Djotodia kuwa rais na kumfanya kiongozi huyo kuwa Rais wa kwanza wa kiislamu kuwa Rais nchini humo.
Mauaji ya kutokomeza jamii dhidi ya raia wa Kiislamu yaliofanyika nchini Afrika ya Kati ambapo Shirika la Haki za Binaadamu la Amnesty International lilisema wanajeshi wa kulinda amani wa kimataifa walishindwa kuyazuwiya mauaji katika nchi hiyo. Amnesty ilisema katika repoti yake ilioitoa imeorodhesha takriban mauaji ya watu 2000 ya raia wa Kiislamu yaliofanywa na makundi ya wanamgambo wa Kikristo yanayojulikana kama dhidi-ya balaka (ANT-BALAKA) ambayo yaliundwa kufuatia mapinduzi ya mwezi wa Machi mwaka 2013 yaliofanywa na kundi la muungano wa waasi la Seleka lenye Waislamu wengi. Katika repoti yake hiyo shirika la Amnesty lilisema mauaji ya kuangamiza jamii ya Waislamu yamekuwa yakifanyika magharibi mwa nchi hiyo ambapo ndiko kwenye idadi kubwa ya wananchi wa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa repoti hiyo jamii nzima za Kiislamu zililazimika kukimbia na mamia ya raia wa Kiislamu ambao walieshindwa kukimbia waliuwawa na makundi ya wanamgambo ya dhidi ya balaka (ANT-BALAKA) ambayo hayana uongozi mahsusi. Shirika hilo limesema mashambulizi dhidi ya Waislamu kwa nia iliotamkwa wazi ya kuiondowa jamii yao nchini humo yalifanyika kutokana na wapiganaji wengi wa dhidi ya balaka (ANT-BALAKA) kuwaona Waislamu kuwa wageni ambao walipaswa kuondoka nchini humo au wauliwe.Shirika hilo la kimataifa la kutetea haki za binadaamu katika report yake liona kwamba makundi hayo yalifanikiwa kutimiza malengo yao hayo ambapo Waislamu wamekuwa wakilazimishwa kukimbia nchi hiyo kwa idadi iliyoongezeka. Mfano mbaya tu ni pale Amnesty ilipo towa orodha ya mauaji kuwa ilikiwa imefikia 60700 na kutoa wito kwa vikosi vya kulinda amani vya kimataifa vilioko nchini humo kuchukuwa hatua za haraka kukomesha mauaji na kutaka udhibiti wa makundi ya dhidi ya balaka (ANT-BALAKA) kwenye mitandao ya barabara wa nchi hiyo na kuweka wanajeshi wa kutosha kwenye miji ambapo Waislamu wako hatarini. Mauaji hayo yalikuwa yakutisha na watu wengi waliuwawa kama kuku.
Hata hivyo Michel Djotodia alilazimika kujiuzulu mwaka 2014 kufuatia shinikizo kutoka kwa jumuiya ya kimataifa kwa kushindwa kuwadhibiti waasi wa kundi la Seleka waliokuwa wakifanya maovu kote nchini yakiwemo mauaji, ubakaji na uporaji wa mali. Na nivyema tukalijua chimbuko la kundi hili la Seleka angalau kiufupi.
KIKUNDI CHA WANAMGHAMBO WA KIISLAM CHA SELEKA (MUUNGANO).
Neno "Seleka" ni neno linalotokana na lugha ya KISANGO lenye maana ya "Muungano" katika kiswahili, kimsingi kundi hili liliundwa mwaka 9/2/1992 kutoka kwa vikundi vidogo vya waislam wenye asili ya nchi ya Chadi waliojulikana kama "islamic for central Africa" (islamiq pour le Benefricq) waliotaka kuwepo na usawa katika dini na hii ilitokana na kuwepo na unyanyasaji wa jamii ya waislam inayopatikana magharibi mwa nchi hiyo kitu kilichopelekea kuwepo na madai ya mda mrefu ya kusaulika kwa jamii hiyo ya waislam wa magharibi mwa nchi hiyo.
Kulipo enea muamko huu idadi kubwa ya vijana wakajiunga na lakin baadae kikundi hicho kilipigwa marufuku na Rais wakipindi hicho Angel Felix Patasse. Kutokana hatua hiyo kuzuiwa ilizidisha hali ya kutafuta kujipanga kwa kikundi hicho na baada vilibadili njia ya mapambano na kuundwa kama vyama vya siasa ikiwapo chama cha kwanza kuundwa cha waislam kilichoitwa NAP kilichoongozwa na Jean Jacques Demafouth mpaka mwaka 9/2/2012 kilipo ungana na chama kingine chenye milengo kama hiyo cha CPSK na kuanza madai ya kutaka waislam washilikishwe kwenye utawala wa nchi hiyo ambayo toka uhuru jamii ya wakristo ndio imekuwa ikishika hatamu.
Hata hivyo tarehe 20/8/2012 vyama vitatu vya kidini ya uislama vya CPSK, CPJP na UFDR viliungana na kuzaa chama cha SELEKA (muungano) ambacho kilikuwa chama cha chenye muundo wa wanamghambo kilicho ongozwa na Michel Djotodia kama mkuu wa kikosi hicho huku kiongozi wa Jeshi hilo la mghambo akiwa bwana Joseph Zoundeiko. Na mapambano yaliendelea mpaka walipo fanikiwa kumuundoa madalakan Bozize na Michel Djotodia kujitangaza kuwa rais. Lakin Kikosi cha Seleka kiliendelea kilindima mitaani na kuendeleza mauaji kwa jamii ya kikristo na kusababisha vifo, ubakaji na wizi wa mali mwaka 2013 Rais Djotodia alitangaza kukivunja kikundi hicho lakini badhi yao walikaidi na kubakia mitaani.
Ni wakati huo kundi la waasi la kikiristo la Anti Balaka lilipoundwa na kuanza mashambulizi makali ya kulipiza kisasi na kusababisha mauaji ya maelfu ya watu na mamilioni wengine kuachwa bila ya makaazi katika taifa hilo maskini. Pia ni busara katika mantiki hili tukalifahamu kikundi hiki cha Ant balaka.
KIKOSI CHA WANAMGHAMBO CHA KIKRISTO CHA ANT-BALAKA (DHIDI YA BALAKA).
Hichi ni kikosi kilicho amua kujibu mapigo ya mauaji yaliyokuwa yakifanya na kikosi cha Seleka dhidi yao. Asili ya kikosi hichi ni mji wa Fula mkoa wa Boali na kiliundwa mwaka 1990 kikiwa kama kikosi cha ulinzi na amani katika vijiji vya mji wa Fula ulio kuwa unavamiwa na wezi mala kwa mala. Kutokana na kuwepo kwa vuguvugu la udini uliopelekea kuiondoa serikali ya wakristo walio wengi iliyo kuwa inaongozwa na Francos Bozize ndipo kikundi hicho kilikjikusanya chini ya kiongozi Levy Yakete na kuanza kujibu na kulipiza kisasi ya mauaji yaliyo tekelezwa na Kikosi cha Seleka na ilipo fika mwaka 7/12/2013 tayali mauaji ya dhid ya uislam yalianza kutapakaa karibu sehemu zote za nchi kikosi cha ANT-BALAKA walitekeleza mauaji na kisha kula nyama za maiti ya binadamu. Kufatia hali hiyo mauaji yaliendelea nchi nzima mpaka duru za kimataifa zilipo ingilia kati na kufanikiwa kuzima mauaji ya kutisha ambayo yalikuwa yakielekea kuwa mauaji ya halaiki.
Wachambuzi wanatilia shaka mazungumzo yaliyo fanyika kutafuta amani ya Nairobi na hawana imani juu ya uwezo wa makundi hayo mawili ya waasi kutekeleza yaliyofikiwa katika katika azimio la amani la Nairobi (Nairobi Peace convetion) katika nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.
HALI YA SIASA BAADA YA MACHAFUKO.
Iwapo chaguzi hizo za Urais zilikuwa shwari, na zilifanyika kwa amani huenda hatua hiyo ikawa mwanzo mpya kwa Jamhuri ya Afrika kati ambayo imezongwa na mapinduzi ya serikali, ghasia na msukosuko tangu ilipojinyakulia uhuru kutoka kwa Ufaransa zaidi ya miongo mitano iliyopita. Katika uchaguzi ulifanyika Wagombea wawili waliogombea urais wote walikuwa mawaziri wakuu wa nchi hiyo na waliahidi kurejsha usalama na kuimarisha uchumi katika taifa hilo lenye utajiri wa madini lakini linakumbwa na umaskini mkubwa. Katika Duru ya kwanza ya uchaguzi mkuu uliofanyika mnamo mwezi Desemba mwaka 2013, na Waziri mkuu wa zamani Anicet Georges Dologuele, kwa kupata asilimia 23.78% ya kura. Dologuele almaarufu "Bwana Msafi" mwenye umri wa miaka 58 anasifika kwa kujaribu kuifanyia mageuzi sekta ya fedha nchini humo wakati alipokuwa Waziri mkuu.
pia upande mwingine Faustin Archange Touadera ambaye pia ana umri wa miaka 58, Professa wa somo la Hesabu na Waziri mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati aliibuka wa pili katika duru hiyo ya kwanza ya uchaguzi kwa kupata asilimia 19.4 ya kura zilizopigwa. Mbali na kumchagua Rais, wapiga kura walishiriki katika uchaguzi wa marudio wa bunge ambao pia ulifanyika tarehe 30 mwezi Desemba mwaka 2014 lakini ulifutiliwa mbali kutokana na madai mengi ya kuwepo udanganyifu katika uchaguzi huo. Wagombea 1,800 waliwania viti 105 vya bunge la nchi hiyo. Uchaguzi wa duru ya pili wa Urais ulifanyika kwa kinyang'anyiro kikali kati ya wagombea hao wawili. Dologuele alipata uungwaji mkono kutoka kwa mgombea aliyeibuka nafsi ya tatu katika duru ya kwanza ya uchaguzi huku Touadera akiungwa mkono na wagombea 22 walioshiriki katika uchaguzi wa Desemba.
uchaguzi huo ndio ulikuwa wa kufanya maamuzi muhimu, kwani Rais ambaye angeshinda ndio ange hudumu madarakani na kutakiwa kulijenga tena taifa hilo na kulejesha matarajio mengi kutoka kwake. Raia Emilienne Namsona ambaye nilipata kuzungumza nae anayeishi katika kambi ya wakimbizi ya M'poko alinieleza kwa kusema "Rais mpya anapaswa kuwapokonya waasi silaha ni jambo muhimu sana ili wao raia waweze kurejea makwao na kuishi kwa uhuru na amani". Uchaguzi huu ulimfanya Faustin Archage Touadera kushinda na kuwa Rais wa awamu ya saba (7) wa taifa hilo changa kiuchumi Afrika.
Rais Faustin-Archange Touadera alikula kiapo cha kulinda katiba ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na kurejesha amani nchini humo kipindi akitawazwa kuwa Rais. Vilevile alihahidi kutekeleza vyema majukumu yake bila ya kuathiriwa na mitazamo ya kikabila au kidini. Faustin-Archange Touadera ambaye alikuwa mwalimu wa somo la hesabati aliwashangaza wengi baada ya kupata ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Februari 14 . Hivi sasa baada ya karibu miaka mitatu ya mapigano na vita vya ndani, wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wana matarajio ya kushuhudia tena amani na usalama nchini humo. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, wataalamu wa mambo wanasisitiza kuwa ukosefu wa usalama na amani ndiyo changamoto kubwa inayoikabili serikali mpya ya Bangui.
Kwa msingi huo inaonekna kuwa, miongoni mwa majukumu muhimu zaidi ya rais mpya wa CAR ni kurejesha hali ya utulivu na mapatano ya kitaifa. Japokuwa ni kwa muda sasa ambapo vita vimekomeshwa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati lakini mapigano ya hapa na pale yangali yanashuhudiwa katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo hasa maeneo ya mji wa Bangui na magharibi mwa nchi hiyo yaliyo na wakazi wengi wa kiislam.
Siku chache zilizopita wakati wa Rais wa serikali ya mpito ya Jamhuri ya Afrika ya Kati Bi Catherine Samba-Panza alikiri kuwa hakufanikiwa kuyapokonya silaha makundi yote ya wanamgambo na kueleza kwamba, ana matumaini serikali mpya itapata ufumbuzi wa matatizo mawili makuu ambayo ni tatizo la "ukosefu wa usalama" na "silaha zinazomilikiwa na makundi ya wanamgambo". Pia Mgogoro wa chakula, hali mbaya sana ya kibinadamu hususan watoto na wanawake, matatizo ya kiuchumi na umaskini ni changamoto nyingine zinazoikabili serikali mpya ya CAR.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon pia ameeleza kusikitishwa na mashaka yanayowasumbua watoto katika Jamhuri ya Afrika ya Kati kutokana na ukati wa aina mbalimbali. Watoto wa nchi hiyo wamekuwa wahanga wa ukatili wa kingono uliofanywa na askari wa kulinda amani waliotumwa kuwalinda. Maelfu ya watoto wadogo pia wameuawa katika mapigano ya ndani na waliookoka wameshuhudia mauaji ya kutisha, suala ambalo yumkini likawasababishia wengi miongoni mwao matatizo ya kinafsi ya kisaikolojia.
Kwa msingi huo kuna haja ya kutiliwa maanani zaidi hali ya watoto wadogo na kuanzishwa vituo vya elimu vyenye suhula za kutosha kwa ajili ya kizazi kipya cha nchi hiyo iliyoathiriwa na vita. Ni vyema kukumbusha hapa kuwa Jamhuri ya Afrika ya Kati inasumbuliwa na hali mbaya sana ya uchumi licha ya kuwa na utajiri wa madini kama almasi na dhahabu. Idadi kubwa ya vijana wa nchi hiyo hawana kazi na nchi hiyo haina miundombinu mizuri ya uchumi na ustawi. Tukiachia mbali hayo yote kwa sasa nchi hiyo inasumbuliwa na uhaba wa chakula. Mkurugenzi Mkuu wa shirika la WFP alisema kuwa Jamhuri ya Afrika ya Kati inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa chakula kwa kadiri kwamba, nusu ya watu wa nchi hiyo wanasumbuliwa na njaa. Kwa vyovyote vile serikali mpya ya Jamhuri ya Afrika ya Kati itakuwa na kibarua kikubwa cha kushughulikia matatizo mengi ya nchi hiyo na kuhakikisha angalau inapunguza machungu na mashaka ya watu wa nchi hiyo.
Mwisho japo sio kwa umuhimu wae ikumbukwe kuwa Jamuhuri ya Africa ya kati ni nchi yenye utajili wa madini ya diamond, dhahabu, Uraniam na Zink imeshindwa kufaidi rasilimali zake kutokana na kuwa na utawala wa kipandikizi kutoka utawala wa awamu ya kwanza na utawala wa kidikiteta ulibujikwa na wizi na ubane wakati wa utawala wa Bokassa. Utawala wa Patasse na Bozize ulikuwa utawala wa kiufisad na ubaguzi na ubinafsi. Historia ya nchi hiyo imekuwa chafu mpaka wakati wa mauaji ya kidini yaliyofanyika hivi karibuni. Sasa utawala mpya unatumainiwa kurejesha hali ya amani na kuleta maendeleo ya taifa hilo.
•Maswali ya kujiuliza Je sisi kama Tanzania tunalakujifunza kutoka nchi hiyo? Kama ndio au la! Na je Tanzania tunahaja ya kupenyeza duru zetu za ushawishi katika nchi hiyo?.
"Mungu ibriki Afrika, Mungu ibariki Jamuhuri ya Afrika ya kati, Mungu wabaliki watu wa Afrika ya kati"
Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu.
copy rights reseved
written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika kwa mawasliano
Comred Mbwana Allyamtu
Kwa Tanzania
+255679555526.
+255765026057.
Kwa Rwanda
+250733153930
+250788214234
Kwa DRC
+243 977 860 824
Email- mbwanaallyamtu990@gmail. Com