Jamaa aliyefanya uwindaji wa Mamba hana kosa; Sababu hizi hapa

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,818
5,420
Kiuhalisia jamaa aliyefanya Poaching hana kosa kwa Mujibu wa kanuni asilia kwa sababu Mnyama kama Mamba yupo kwenye Top of Food Chain, yani ni mnyama hasiyekuwa na Natural Predator au competition kutoka kwa Predators wa jamii nyingine tofauti na wanyama kama Simba, Chui, Duma na Fisi ambao kila mara itabidi wapigane wakikutana kwa ajili ya Food Competitions. Mnyama kama mamba hana food competitions kwenye maeneo anayoishi, na yeye ndio Top predator kwenye eneo analotawala, kwa sababu Kiboko yeye hali nyama anakula Nyasi hivyo kumfanya Mamba kuwa Mwindaji pekee kwenye maeneo ya mito na mabwawa.

Kwa sababu Mamba hana competitions kutoka kwa Predators wengine inapelekea uzao wao kuwa Undisturbed ukiachilia mbali mayai wanayotaga ambayo mara nyingine uliwa na wanyama wengine kama ngedele au nyoka, au wanyama wengine waokula mayai ya mamba.

Kitendo cha Mamba kuwa on Top of food Chain without competitions, kinapelekea mamba kuwa natural predator asiyesumbuliwa sana, hivyo wanazaliana sana na wanakufa natural death. Sasa hili kuweka balance ya mamba wasiwe wengi kupelekea kuleta madhara kwa watu na kwa wanyama wengine ambayo mamba wakiwa wengi basi watapeleka wanyama wengine kutoweka basi Serikali ikaamua kurasmisha uwindaji (legal Poaching) kwa ajili ya kupunguza wanyama amabo kimsingi wakizidi sana mbugani wataleta shida na kupelekea kutoweka kwa wanyama wengine au kusababisha madhara ya kimazingira au kwenye maisha ya watu. Na miongoni mwa wanyama wanaoruhusiwa kuwindwa basi ni Mamba kwa kimombo Crocodiles a.k.a Israel.

Hapo chini ni jamaa aliyewinda Mamba na kupelekea kuleta maswali mengi kwenye jamii


View: https://www.instagram.com/reel/C1VJGRppaYu/?igsh=eWwwMjFuYzgxM3No
 
Back
Top Bottom