ILEMELA Mwanza: Mama aua mtoto wake aliyekataa shule

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Mkazi wa Nsumba katika Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza Joyce Mathayo (33) anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kumpiga mtoto wake Mathayo Manisi (12) na kumuua kwa kosa la utoro shuleni

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini hapa jana alisema tukio hilo lilitokea Januari 11 mwaka huu saa 4 asubuhi

Alisema Joyce alikamatwa na polisi baada ya kumpiga fimbo mtoto wake huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu sehemu mbalimbali za mwili na kusababishia kifo chake, kitendo ambacho ni kosa la jinai

Kamanda Msangi alisema siku ya tukio, mtoto huyo alimkatalia mama yake kwenda shule na kusema hataki shule tena, ndipo mama huyo alipopatwa na hasira na kuanza kumpiga fimbo sehemu mbalimbali za mwili na kusababishia kifo muda mfupi baadaye

Alisema baada ya mtoto huyo kufa, wananchi waliamua kutoa taarifa kituo cha polisi na polisi walifika mapema kwenye eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa

"Mtuhumiwa yupo katika mahojiano na polisi, pindi uchunguzi utakapokamilika atafikishwa mahakamani, mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na timu ya Madaktari kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Sekou Toure na tayari umekabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya maziko".alisema

Kufuatia tukio hilo la kusikitisha, Kamanda Msangi ametoa wito kwa wazazi kuwalea watoto wao katika maadili mema na nidhamu kwa kuwaelimisha mambo mazuri na mabaya ili kuepusha kutoa adhabu za vipigo kwa watoto kwa kujenga familia bora isiyo na ukatili.

Chanzo : HabariLeo
 
Inna Lilah wa inna Illahii Rajiuun,poleni wafiwa.Inahuzunisha.
 
Haina haja ya kumkamata mama hiyo ni bahati mbaya na kwanza ni jukumu la mama kumpiga mtoto pale anapoleta upumbavu hiyo kufa imetokea tu
ukapimwe wew uyo jela miaka 30 fuatilia ulete mrejesho hapa jf bloodful kabisa ww
 
Mkuu.. ungemfanya awe sugu tu hapo, nadhani dogo ni utoto wake na michezo mingi ndo maana akimwambia vile mama yake kuwa hataki shule

Mama ilibidi angechukua hekima zaidi kwa kumjenga kiakili zaidi kuliko jazba ambazo zimepelekea kifo chake
Hasira, hakunuia kumuua, nampa pole sana.
 
Inasikitisha kwa kweli. ..yeuwii jamani. .dah!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…