JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,661
- 6,395
Matukio makubwa yanayoendelea hapa nchini Tanzania ni kuhusu mauaji, wapo wanaowaua wengine na wengine wanajiua, daa! Bongo hali mbaya.
Lakini upande wa pili kuna kesi na taarifa kadhaa kuhusu askari polisi kuua raia na wengine kuuana wao kwa wao.
Mtwara kule kuna kesi ya askari kuua mfanyabiashara, siwezi kuliingilia ndani suala hilo kwa kuwa lipo mahakamani kwa sasa, upande wa pili mkoan Kilimanjaro pia kuna sakata la madai kuwa askari walimuua askari mwenzao kisha kudanganya alifariki kwa ajali ya bodaboda.
Baadaye ikaelezwa kuwa eti alipigwa risasi kwa bahati mbaya na askari mwenzake, na bla!bla! nyingine kadhaa.
Kwa taswira hiyo inawezekana kuna mambo mengi yanaendelea mtaani kuhusu Jeshi la Polisi Tanzania, nadhani ni vema mamlaka husika kuanzia kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro kujitafakari kwa kina kwa hiki kinachoendelea.
Kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu jeshi hilo, raia wengi wanashindwa kuwa huru kutoa hisia zao, lakini serikali na mamlaka husika zinatakiwa kutazama matukio haya kwa jicho la ziada kabla mambo hayajawa mabaya zaidi inawezekana kuna makubwa Zaidi ya haya machache yaliyoripotiwa.
Mwaka jana Rais Samia Suluhu alitoa angalizo kwa Sirro kufuatilia kinachoendelea hadi askari wengi kutamani kwenda kitengo cha trafriki, akamwambia achunguze kwa nini! Kwani unadhani Wabongo hawajui kwa nini vijana wengi wanapenda kwenda trafiki ni kwa kuwa wanajua kuna maslahi ya ‘shortcut’ ambayo siyo halali.
Hiyo ni ishara wazi kuwa kuna ‘madudu’ mengi yanaendelea kwenye jeshi hilo na mamlaka za juu zinajua.