HUZUNI: Watanzania kuwaaga Watoto, Waalimu na Dereva wa ajali ya Karatu, uwanja wa Sheikh Amri Abeid

Huwa nakaa nafikiria wale wanaume walijitoa kwa hali na Mali kuzitoa zile maiti zote kule bondeni au korongoni ndani ya gari bila kujali chochote kile!!

MUNGU ndiye mlipaji wa kila kitu hapa duniani,Nasema MUNGU na awalinde na kuwasahaulisha yote mliyopitia kwa wakati najua nia yenu ilikuwa ni moja tu kuzitoa maiti za wapendwa Watoto wetu.

Kuna wengine inaweza kuwa ndiyo mwanzo wa kupata tatizo lingine kisaikolojia vijana hao nao wanahitaji ukaribu pia wa kisaikolojia maana kuna picha ambayo haitafutika ktk maisha yao.
Ndio maana ya kua men
 
Huu ujingaujinga wa kukoswa utu na kutanguliza maonyesho nalo ni tatizo lingine la kitaifa. Tangu lini tanzia ikawekwa lipicha la mtu aliye hai? Huu ni msiba wala si habari za unazi wa mavyama. Gambo kachemka sana kuweka lipicha lake hapo na kama anawashauri wafanye haraka sana kumwambia atoe huo uchafu wake.

Maumivu ya wazazi wa marehemu ni makubwa kuliko tunavyoweza kufikiri. Ni Mungu pekee ndiye awezaye kujua leo na kesho.
Tumwombe Mungu awafariji wafiwa na pia aziweke roho za watoto pamoja na walimu hao mahala pema peponi, Amina.
 
Hivi kuna umuhimu wa mkuu wa mkoa kujionyesha kwa kubandika picha yake kwenye mambo ya msiba kama haya! Hawa wana siasa ni ovyo kweli kweli. Si wangeweka picha za marehemu au hata nembo ya shule? Kichefuchefu!
Jamani Picha za wanafunzi wote kweli ktk document hiyo ingetosha ....Kwani picha yake ina madhara gani kwa mfano.....
 
Kiukweli Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuweka picha yako ktk Tangazo la utaratibu wa maombolezo hapo kesho na kuweka maneno ya dini na upande mwingine nembo ya Taifa Tangazo hilo halija kidhi vigezo vya matangazo ya Serikali.

Kuna wengi tu hatujapendezwa na mtengenezaji wa Tangazo kama hilo ktk kipindi ambacho Taifa linaomboleza.

Hata ma ADM wa magroup wameungana na wafiwa kwa kuweka mishimaa au picha ya Watoto iliyopigwa kabla basi hata ungeweka picha ya shule yao kuliko kuweka picha yako wewe ambaye uko hai.

Sio ishara nzuri sana kuweka picha yako ktk msiba mkubwa kama huu kitaifa Mkuu wa Mkoa.
 
Jamani Picha za wanafunzi wote kweli ktk document hiyo ingetosha ....Kwani picha yake ina madhara gani kwa mfano.....
Wasn't necessary kuweka picha za Marehemu kwa kuwa idadi ni Kubwa.

Lakini hakupaswa kabisa kuweka Picha yake yeye katika Tangazo hilo la Msiba.

Endeleeni Kumpotosha kwa Kuwa Ndiyo hulka yenu kuu kwa kuwa mkono unaenda kinywani, Hicho alichokifanya ni Upuuzi na Upunguani Mkubwa kabisa.
 
Vijana wakipewa nafasi wanawekeza nguvu zao katika kuuza sura na kutaka kuwa habari badala ya kuwa watendaji wazuri!
 
Wasn't necessary kuweka picha za Marehemu kwa kuwa idadi ni Kubwa.

Lakini hakupaswa kabisa kuweka Picha yake yeye katika Tangazo hilo la Msiba.

Endeleeni Kumpotosha kwa Kuwa Ndiyo hulka yenu kuu kwa kuwa mkono unaenda kinywani, Hicho alichokifanya ni Upuuzi na Upunguani Mkubwa kabisa.
Sawa mkuu...kosa amelifanya.
 
View attachment 505748

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe Mrisho Gambo, kesho Jumatatu ya tarehe 08/05/2017, Makamu wa Rais wa JMT, Bi Samiah Suluhu ataongoza watanzania wote ktk maombolezo ya msiba wa wanafunzi, walimu na dereva wa shule ya Lucky Vincent waliofariki kwa ajali ya basi wilayani Karatu hapo jana.
Japo tumeelezwa kuwa ni Makamo wa Rais ndie ataongoza Watanzania kuwaaga wenzetu hawa, kuna kitu kinaniambia kuwa pia kuna mtu fulani muhimu ataguswa na msiba huu mzito na kesho asubuhi ataamkia Arusha na atatinga Sheikh Amri Abeid as a surprise!.

Paskali.
 
Utakuwa ni muendelezo wa Maigizo ama tuseme pretending behaviour ya ajabu kabisa.

Kwani kama kweli ameguswa kutoka moyoni angeweza kuahirisha shughuli zake zote zilizo kwenye ratiba yake ili ashiriki ibada ile kwani Msiba ule ni Mkubwa sana.

Hakuwa na sababu yotote yakufanya such unpredictable "dramatic" action.
 
Pole nyingi kwa wazazi ndugu na jamaa,
inahitajika subira na uvumilivu mkubwa ktk kipindi hiki kigumu!
 
Japo tumeelezwa kuwa ni Makamo wa Rais ndie ataongoza Watanzania kuwaaga wenzetu hawa, kuna kitu kinaniambia kuwa pia kuna mtu fulani muhimu ataguswa na msiba huu mzito na kesho asubuhi ataamkia Arusha na atatinga Sheikh Amri Abeid as a surprise!.

Paskali.
Paskali. Nakuuliza swali (sijui hata kama una jibu). Huko ikulu hakuna watu waliobobea kwenye mambo ya taasisi ya urais? Huu msinba sio mchezo ati. Nitashangaa sana sana kama rais mwenyewe hatahudhuria. Mimi nilikuwa nategemea hata angetoa hotuba maalum!
 
Back
Top Bottom