Huzuni: Mama Mzazi amchoma mwanae kwa kudokoa Tsh 1,000

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Hii habari ya huyu Mtoto alopost Sam imenigusa sana, Hivi kwanini wanawake wa siku hizi wamezidi kwa ukatili na roho mbaya? Wanawake wanajaribu kuwafanyia ukatili waume zao sasa wamehamia kwa watoto.
Badilikeni wakina mama.

"Mama mzazi amfanyia ukatili mwanae wa kumzaa kwa kumfunga mikono yake miwili kisha kumchoma moto kwa madai ya kuiba shilingi 1000 tu... Sam Mahela nimeinyaka hili tukio.

Dah inatia huruma sana"
 
Dah, binadamu wamepoteza imani na utu. Hapo anaweza kumsababishia ulemavu wa maisha huyo mtoto. Sijui ningemfanyaje huyo mwanamke kama angekuwa ni mwanangu ndio katendewa hivyo.
 
Dah..! kuna wanawake wana roho ngumu. Mungu aniepushe na hasira za kiasi hicho kwa mwanangu
 
Kuna watu watasema hali ngumu ya maisha, Hapana huu ni ukatili na roho mbaya havihusiana na hali ngumu ya kimaisha.
 
Masikini hawatakaa waingie Mbinguni.

Imebainika wanatenda dhambi kuliko matajiri.
 
Nimeumizwa sana na taarifa iliyoonyeshwa na ITV ya mtoto aliyeunguzwa na mama yake kwa sababu kaiba sh.600!! Ninayaandika haya nikiwa ninalia,tumbo la uzazi linaniunguruma,nimekabwa na kitu shingoni baada ya kusikia maelezo ya mama mzazi wa huyo mtoto,jamani tunaelekea wapi?
tunakuwa na roho za kinyama,sauti ya mtoto akilia kwa maumivu makali, tena yaliyosababishwa na mama yake mzazi!!!!kama siyo sisi nani awatetee watoto hawa? Taasisi husika litizameni hili kwa jicho la 3!!
 
Mungu amponye mwili Na Roho mtoto huyu,wakina mama tuwalee watoto kwa upendo na kuwafundisha kutosheka kujua kukosa Na kupata Na kuridhika Na mahitaji tunayo wapa Na sio matakwa yao Na kila wanachotamani.
 
Hivi ni hasira gani hizi jamani?! Huyo mama akapimwe kwanza akili ndio hatua zingine ziendelee..., inatia uchungu sana. Hivi huyo mtoto hana baba? Atakaemfanyia mtoto wangu ushenzi wa aina yeyote ule, sitojali ni nani, nitakaanga vidole vyake na kula kama mishkaki, please, children are to be protected at all costs..!
 
Kama sio mimi Mama ni nani amtetee mwanangu? Sasa kwanini mimi niwe sehemu ya hao watakaomsababishia Maumivu ambao mimi natakiwa nimtetee,nimpiganie nipambane kwa niaba yake!? Allah nijaalie niwe na moyo wa woga kwa kizazi changu na hata wale wasio kizazi changu
 
Yaani ingelikuwa ni mama wa kambo,sijui ingekuaje.Jamani ubaya hauna kwao,hauna mama mzazi wala wa kambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…