Habarini Wadau,
Kuna hizi tabia za kipumbavu ambazo unakuta mwanaume anazifanya halafu haipendezi aisee,tena ni tabia za kikekike na za kitoto. Wewe kama Mwanaume na sio mvulana acha kufanya yafuatayo,tuwaachie warembo:-
1) Mwanaume kulalamika hovyo na Kuzira. wewe unalalamika halafu wa kike afanyaje? Ukipatwa na jambo si unagangamala mazee na sio kulialia? Mtoto mdg afanyaje? Acha hizo mambo.
2) Mwanaume kuhonga kisha kujutia/kulalamika. Sasa kama umeshamuhonga mwanamke kwa kuamua mwenyewe na aidha kakupa mzigo au hajakupa...ukilalamika au kuhadithia masela inasaidia nini? Kuhonga ni kawaida na unapohonga basi fanyeni yenu na dem wako kulalamika inasaidia nini mkuu?
3) Kutumia vijimaneno vya kike mfano:
-Haloo,
-Mie....
-Fyuu...
-lol..
-Badala ya "S" mwanaume anatumia "X"
-mara "Utantaka"
-au kwenye Okay eti "K"
Dume mwenzio anakutumia message mpaka unajiuliza aliyeandika ni yeye au mtoto wake?au karibia anakuwa shosti?
Hapo hata ukitongoza mwanamke akakukataa ni haki kwasababu anakuona ni kavulaaana au wakike mwenzie.
4) Kuomba ushauri kwenye vitu vidoogo na visivyo na umuhimu. Hii ni hapahapa jamvini kuna wanaume wanaomba ushauri kwenye mambo ambayo hata mtoto wa form two anaweza kutatua jambo hilo.
5) Kujisifia sanaa kwenye issue ambazo sio za msingi sana,mfano
-sura, umbo, kupendwa na mabinti, kugegeda n.k
Mimi nafikiri sifa tukufu kwa mwanaume ni kutafuta pesa na kumanage majukumu ya nyumbani.
Jistukie bana mkuu.
NAWASILISHA.