Humphrey Polepole, fikisha ujumbe huu ngazi za juu

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Hili ni ombi-amri. Ni kwa maslahi mapana ya chama chetu na hata Serikali iliyoundwa na chama chetu cha Mapinduzi. Katika kuonesha kuwa CCM na Serikali ya awamu hii ya tano zimemiliki kila idara ya 'mechi' hii ya kisiasa Tanzania, ni vyema jambo hili likafanyika.

Nakuomba na kukuagiza kufikisha ujumbe huu kwa wahusika wa kiserikali na kichama. Umefika wakati wa kuwa na BUNGE LIVE. Kuanzia tarehe 31 mwezi huu, Bunge litaanza vikao vyake Dodoma. Ni wakati wa kuruhusu BUNGE LIVE.

Tunataka kuwaona Mawaziri wetu wakijibu majibu mujarabu bila tabu. Tunataka kuwaona Wabunge wetu wakijenga hoja za haja na za kuleta faraja. BUNGE LIVE litarudisha ari ya Wabunge wetu ambayo imeporomoka vya kutosha na kutisha.

BUNGE LIVE litatupa 'ujiko' CCM na kusahaulisha katazo la mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa nchini. BUNGE LIVE litatuonesha wanaCCM jinsi tunavyojua mambo na siasa. Bunge ni uwanja mkubwa zaidi wa kisiasa. Tuutumie kwa kuonesha BUNGE LIVE.

Mwafaaa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)
 
Mzee tupatupa habari za asubuhi mzee wangu.
Naomba nikukumbushe hilo lichama lenu hakuna atakaekusikia kwa sasa wamebadilika wamechukua tabia za kenge. Chama chenu kimegeuka kuwa watawala badala ya kuwa viongozi. Mmejawa kibri,chuki,majivuno,unafiki,ukabila,ukanda,udini,ubinafsi na mbaya zaidi mmetawaliwa kwa uongo na matamko hewa.
 
Polepole yupi unamwagiza?
Huyu huyu juzi aliyealikwa kunywa juice za ikulu?
Pole Tupa Tupa maana huyu ni bingwa wa kumsujudia rais sizani km anaweza kusema lolote mbele yake.
 
Umekosa watu wa kutuma, ccm lichama limeshakufa . nasijui unasubili nini kutoka uko
 
Sawa kabisa tume miss utumbo wa Kibajaji ,Serukamba Halima,Musukuma na sasa ameongezeka babaake Halima
 
Kuzuia bunge live kwa kigezo cha gharama ni UONGO mkubwa..

Mnaogopa hoja za wapinzani zenye mashiko zisiwafikie wananchi.

Mnajua fika wabunge wenu wengi wa CCM vichwani hamna kitu.. Hawana hoja, zaidi ni kulala mle ndani na matusi basi.

Rudisheni bunge live muone mtakavyo washiwa moto mle ndani..

Aibu yenu CCM..
 
ukitaka kumtawala mtu yeyote duniani..
1:mjengee hofu juu ya maisha yake na shughuli zake
2:mnyime elimu na uhuru
3:anza kumkejeli kwa majivuno yako na kujipaisha kwa kujipa sifa zisizostahili..

hayo ndo ccm inawafanyia watz walio wengi..
 
Kwa nini CCM wamekuwa waoga kiasi hiki? Maana mwoga huweza kikimbia hata kivuli chake mwenyewe! Wananaogopa mikutano ya kisiasa. Sawa, lakini hata bunge mubashara!!!!
 
Wanazuia bunge live eti watu wakafanye kazi. Huwezi kupingana na sauti ya wengi sauti ya Mungu. Haya sasa, wamelima mvua hakuna, wakija kwako unasema huna shamba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…