Ndugu zanguni goja nitolee mfano wa hukumu ya Mh Daniel Yona na mwenzake, eti wamehukumiwa kutumikia kifungo cha nje na kufanya kazi za kijamii mtaani pamoja na tuhuma zote zile nilizokuwa nikizisikia dhidi yao!. Kadhalika na kesi zingine zinazo fanana na hayo makundi niliyotaja hapo juu. Mwenye kumbukumbu anisaidie, nimatajiri gani na vigogo wepi wamekwisha tumikia vifungo vikubwa kama wanavyo tumikia ndugu zangu walio iba kuku, simbilisi, mbuzi n.k. Mmmm naomba wanajamii forum niaminishe kuwa hata matajiri na vigogo serikalini wanaweza kufungwa kama watu wengine kulingana na makosa yao, vinginevyo nitaendelea kuamini kuwa ukiwa na fedha au ukawa na nafasi kubwa serikali huwezi kuguswa na mahakama zetu, na hata ukiguswa una nafasi ya kujadiliana nazo ukapangiwa adhabu unayoona inafaa kwako.