Mbona huku Mwanza tulio changua chama chetu mambo poaWakuu ikiwa imebakia siku moja lile zoezi la bomoa bomoa liendelee kuna kesi ya kuomba kuzuia zoezi hilo mpaka kesi ya msingi kusililizwa.
Tafadhali kwa yoyote mwenye updates asisite kushea na jamii ya watanzania
Natanguliza shukrani.
============
View attachment 314853
Mbunge wa Kinonodon, Maulid Mtulya (katikati) akiwa sambamba na baadhi ya Mawakili wanaosimamia kesi ya kupinga kubomolewa kwa wakazi wa Mabondeni wa jimbo hilo la Kinondoni mapema leo Januari 4, muda mfupi baada ya kutoka kusikilizwa kwa kesi yao ya msingi ya kupinga kubomolewa.
Kesi hiyo ilifunguliwa na Mbunge huyo kwa kwa lengo la kutetea wananchi hao ili haki ipatikane na hatma ya wapi watapelekwa. (Picha zote na Andrew Chale).
Dar es Salaam
Umati wa wananchi wa Mabondeni ikiwemo bonde la Msimbazi, Magomeni Mkwajuni, Hananasifu, Magomeni Sunna, Kigogo na maeneo mengine wa Jimbo la Kinondoni wamefurika kwa wingi mapema kuanzia asubuhi ya leo katika Mahakama Kuu ya Ardhi iliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam kusikiliza kesi ya msingi ya kupinga kubomolewa nyumba zao iliyofunguliwa na Mbunge wa Jimbo hilo, Mh. Maulidi Mtulia (CUF).
Mtulia amefungua kesi hiyo kupinga kubomolewa kwa wakazi hao bila kuwa na njia mbadala ikiwemo kupatiwa makazi mengine kwa wananchi wake yenye usalama zaidi.
Hata hivyoi Modewjiblog iliyokuwa katika eneo la tukio tokea asubuhi, ilishuhudia umati mkubwa wa wananchi wakifurika katika viunga vya Mahakama hiyo kiasi cha kufanya shughuli zingine za mahakama hiyo kusimama.
Baada ya masaa matatu, Jaji wa Mahakama hiyo Kuu ya Ardhi, Mh. Panterine Kente aliweza kusimamia kesi hiyo huku baadhi ya wananchi wakiwakilishwa na wajumbe zaidi ya saba, pamoja na wanasheria wa Mbunge huyo, ambapo maamuzi yalidumu kwa muda wa saa zaidi ya saa moja, na baadae Mawakili wa upande wa Mbunge wa Kinondoni, akiwemo Abubakari Salim aliweza kuutangazia wananchi hao pamoja na wanahabari kuwa, baada ya kupitia vielelezo vyote, kesi hiyo itatolewa hukumu kesho siku ya Jumanne, Januari 5.2016.
“Kwa shauri lililopo sasa linatarajiwa kutolewa jibu kesho Januari 5, Saa tano asubuhi ndio tutapata jibu kamili, kwa sasa tunarudi na tutakutana hapa hapa Mahakamani.” alieleza Wakili huyo.
View attachment 314855 Wananchi wanaopinga kubomolewa mabondeni wakiondoka katika eneo la Mahakama ya Kuu ya ardhi.
CHANZO: Mo Dewji
Pole if my comments zimekuumiza! Sio my intention!Na wewe unajiona unajua kujibu eti kueni akili wewe ndio ukue umekaa na kikoroshobhausomi mtu kuelewa ungesoma ungejua kuwa nimeuliza nataka kuelezwa ila unakimbilia kutetea sijui nini mwisho wa siku na akili ndogo yako unachemsha.
Tanzania hatuna kabila la wahindi.Hizo nyumba zilikuwa za hao wahindi unaowasema kuwa wanakaa na isitoshe waliponyanganywa walipewa waafrica na wao wakauza wakauza kwa wahindi wao wakahamia uswazi..kosa la nani hapo au nani wa kulaumiwa ?
Usikimbilie ukabila na urangi toa hoja ieleweke. Kwani wahindi sio watanzania ?
Kukiwa na utaratibu uliopangika vizuri watahama.
Ya kwako itakuja tu. Usidhani utanusurika. Ewe kiumbe katili.Na zipigwe nyundo mpaka chini!
Juzi kitana alikua anafanyaje??Mbona huku Mwanza tulio changua chama chetu mambo poa
Wewe mbona unaropoka sana?? Mafuriko hata marekani,china,japan n,k yapo,afu nani kakwmbia kuna mafuriko ?miaka yote sisi huku tunaishi hatupati mafuriko ya kuua na hayatotokeaWamaposema hawakupewa sehemu mbona wengine wanasema walipewa au ndio maeneo tofauti yanaongelewa.
Pia huyo Mbunge tuseme mafuriko yatokee wakati ameweka kesibna maafa(Mungu aepushe) atafanyaje?
Pole if my comments zimekuumiza! Sio my intention!
I thought unauliza kwa maana ya kuwashangaa!
Wapo waliokuwa wamelipwa! Hadi sasa kuna nyumba 3500 zilizowekwa x lkn mabwepande kuna viwanja visivyozidi 100 ambavyo walipatiwa wananchi wa Jangwani! Kweli wapo wasiostahiki kulipwa Ila wapo ambao wanastahili kusaidiwa na serikali, wapo watumishi wa serikali wanapaswa aliwajibishwa tena hapo mkwajuni ni less than 2 km kutoka makao makuu ya halmashauri ya kinondoni!
Lkn wenzetu wapo ktk hali mbaya, njia waliyotumia ya mahakama ni njia njema zaidi kuliko zote, kuchoma matairi, kuandamana, kufanya fujo etc vingehatarisha usalama wao na wengine kwa ujumla!
Pole once again kama majibu yangu yanakukwaza!
Wewe mbona unaropoka sana?? Mafuriko hata marekani,china,japan n,k yapo,afu nani kakwmbia kuna mafuriko ?miaka yote sisi huku tunaishi hatupati mafuriko ya kuua na hayatotokea