Habari zenu wadau, wivu ni kitu muhimu katika mapenzi lakini ukizidi huwa unakuwa Tatizo. Nakumbuka ilikuwa mwaka 2012, home tulipata msichana kwa ajili ya kutusaidia kazi za nyumbani yaani housegirl, alikuwa ni binti mzuri japo kwa upande wangu hakunivutia, sababu yeye alikuwa mwembamba wakati mimi napenda mizigo, hivyo sikiwahi kuwaza hata kumuomba papuchi. Tatizo la huyu binti lilikuwa ukifika muda wa hedhi/period/kwenda mwezini ilikuwa balaa, yaani tumbo lilikuwa likimsumbua kupita maelezo, alikuwa halali, yaani anahangaika usiku kucha, mchana kutwa anagalagala na kugugumia kwa maumivu aliyokuwa anapata. Sikujua hasa tatizo lilikuwa nini lakini yeye alidai kila ikifika hedhi hiyo hali lazima imtokee, kwakweli alikuwa anapata shida yule binti, mpaka anatia huruma, mama na majirani walikuwa wakimpa huduma na dawa zake za kienyeji ambazo hazikuwa zikimsaidia saana. Kuona hivyo mimi nilichukua simu yangu na kucheki majina ya mabinti wote ambao niliwasave, na kuidraft message ya kuwauliza kama hali kama hiyo huwa inawatokea? Au mtu anayepatwa na hali hiyo unaweza kumsaidiaje? Wengi walitoa majibu ya kuridhisha isipokuwa binti mmoja ambaye ndio kwanza nilikuwa nimempata kama mpenzi wangu, yeye alisema ntajua mimi mwenyewe jinsi ya kumsaidia huyo malaya wangu, nilijaribu kumuelewesha kwamba ni housegirl wetu lakini waapi binti hakuelewa, na akasema nisimtafute tena kuanzia siku hiyo, nilidhani ni masikhara kumbe mtu alikuwa serious. Basi toka siku ile yule binti hakuwahi kunisikiliza kwa chochote, na mimi mwisho nilikata tamaa ya kumbembeleza na mwisho tukaachana kweli. Basi hivyo ndivyo housegirl alifanya niachwe na girlfriend wangu