Hongera Serikali kwa kuanza kurasimisha ujuzi

Mtini

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
1,491
2,355
Serikali imeanza mpango wa kuwatambua watu wenye ujuzi mbalimbali ambo hawakupata nafasi nafasi ya kuingia darasani (Formal education). Fulsa hii itawafanya watanzania mbalimbali wenye ujuzi na uzoefu kupata vyeti rasmi hatimaye kuweza kuajirika katika mfumo wa ajira rasmi


 
Hongera, nimejaribu kuwapigia nikatumiwa ujumbe huu:
Kama wewe ni fundi ambaye ujuzi wako haukupatikana chuoni, umeandaliwa utaratibu ambao VETA itaupima ujuzi wako na kuutambua kwa kukutunuku cheti. Fomu zinapatikana bure ofisi za Halmashauri za wilaya uliza ofisi ya afisa vijana au afisa maendeleo wilaya. Fani husika ni ufundi magari, ujenzi, useremala, hoteli (yaani upishi na wahudumu wa bar na mahoteli)
 
hilo jambo litafanywa ki ccm badala ya serikali kwa minajiri ya watanzania.


swissme
 
Hapa rushwa itatembea haswa kama kipindi kile cha kubadilisha leseni.

Good observation. But what should we do? Tukae tusipige hatua hii muhimu kwa kuhofia kikwazo hiki ambacho kwa miaka mingi kimeiathiri sana jamii yetu ? HAPANA!

Ni jukumu la kila mmoja kuunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na huyo mdudu "rushwa" kwa nguvu, akili na uwezo weto. Programu hii ni muhimu sana kwa taifa na kwa vijana wetu. Tuna vijana wengi ambao wana ujuzi lakini ujuzi wao hautambuliwi. Kwa hiyo wameshindwa ku-access fursa nyingi kwa maendeleo yao. Maana ujuzi wao hautambuliki (Sio rasmi)

Mafundi wote wenye umri usiozidi miaka 45 na uzoefu usiopungua miaka mitano (5) - watumie fursa hii vizuri. Tarehe ya mwisho kuchukua na kurudisha fomu ni tarehe 25/01/2017

Pongezi kwa serikali.
 

You may be right, but as long as its values is still there and the program can improve the working condition of our you youths (i.e. Help them to have descent employment) then we are not late.
 
Umeeleza vizuri lakini tusikurupuke lazima uandaliwe utaratibu mzuri kuepuka corruption.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…