Hoja kwa Polisi na TRA kuhusu kutoa mizigo bandarini

Marathon day

JF-Expert Member
Jan 31, 2020
641
1,005
HOJA na MALALAMIKO kwa POLICE na TRA kuhusu biashara ya kutoa mizigo Bandarini, Naanza kwa TRA unachangamoto kubwa kwenye kukokotoa malipo ya Wharfage , kunahaja gani kutumia custom value badala ya kutumia CBM kwa mizigo/ magari ya Zambia na Zimbabwe?

Inaleta ukakasi Sana, mteja anakupa kazi unalazimika kumuomba Documents kabla, ili kupata value ya Gari, wakati wangetumia Kukokotoa kwa kutumia CBM ingekua rahisi Sana!! Naomba TRA mkaliangalie hilo, linachangia wateja wengi kuhama Bandari yetu.

Niende kwenye police wetu, mteja ameagiza Gari yake kuja kuichukua anakuja na mke na watoto wake kwa ajili ya kutalii na kufanya shopping , atalala Hotel na shopping Kariakoo kote huko analipia kodi, ataweka mafuta kwenye Gari yake yote na kodi kwa serikali, watahitaji kukodi Dereva kumuendesha mpaka boda, amezalisha ajira kwa vijana wetu.

Tatizo litaanza akiingia barabarani sasa ! police wetu watamkimbilia kama amebeba Bangi, watamwambia Gari hii inaruhusiwa mtu mmoja tuu. hapo atahitajika kutoa rushwa njia nzima. kila km moja ya safari yake. kwanini asihame Bandari kwa kero hii?

Uongozi wa Polisi wetu hasa wa usalama barabarani mkaliangalie na hili, ni kero kubwa Kartika ushindani wa Bandari zetu.
 
Kwa hiyo tunakubaliana kuwa tatizo SIO teknolojia Bali usimamizi mbaya Wa kushindwa kudhibiti wahuni .

Ni wazi kuwa hata angepewa malaika achilia mbali Mwarabu Kama kuna mfumo Wa kupeana ulaji na kuoneana aibu Bado wateja watakimbia
 
Zile gari hazina usajili hivyo zinapaswa pelekwa na dereva pekee.

Ikitokea limepata ajali bima haihusiki na waliokuwa ndani ya gari
 
Back
Top Bottom