Hizi zaweza kuwa sababu za teua na tengua kila kukicha?

bitare

Senior Member
Jul 13, 2023
196
599
Ni kama tengua teua kila siku zaanza kuwa kawaida yani viongozi sasa hivi ni kama wameisha. Zile enzi za kusikia Mkuu wa Mkoa kutumikia kwa kipindi kirefu sasa zimeisha, sijui nini kimetokea.

Niliwahi kumwambia kiongozi fulani kuna baadhi ya vitengo fulani ilifaa viongozwe na wasomi na waliotumikia serikali kwa muda mlefu, ila pia wawe wa makamo kama sio wazee kabisa inabidi uwe na upeo mkubwa ili uweze kupinga hoja yangu.

Wakati sisi tukifikili vijana ndo damu motomoto ila mi hua siamini kabisa katika vijana kwenye baadhi ya nyazifa hasa hizi tatu za Uwazili, Ukuu wa mkoa na Ukuu wa wilaya na hapa ndo huwa najiuliza kwanini Maasikofu wa Kanisa Kanisa Katoliki wote unakuta si tu niwasomi wa Phd, ila pia niwatu wazima wa miaka kati 50 na zaidi, hii sio pia ndio siri yamafanikio ya taasii hii?

Ndiyo maana ukiona Mkuu wa Mkoa anasimama nakumpa maelekezo Raisi wa Nchi kua nayeye nimkatoliki na atawashugulikia wale wanaojalibu kumkwamisha unajiuliza huyu kweli amekulia kwenye ukatoliki mpaka ajitokeze nakutaka akabiliane na maaskofu?

Hivi vyeo vinahitaji si tu wasomi bali watu wliopevuka kiuongozi na wenye busara.
 
WATANZANIA walipiga kelele nyingi sana baada ya januari na maharage na bodi mpya kuteuliwa wakapuuzwa sasa matokeo yameprove wamefeli vibaya nchi iko gizani

Aibu kwa samia na mamlaka yake ya uteuzi waliteuwa kimihemko badala ya kuangalia weledi ona sasa kamrudisha Mhandisi kuwa Mkurugenzi

Na bodi kaiweka Mwenyekiti mpya

Rais apunguze kuziba masikio 😕
 
Samia kachelewa sana kulijua hili. Bado wateule vichwa maji wako wengi sana
Sana yani lakini si anasema kaziba masikio muache atashuhudia mengi kama hili la TANESCO hali imekuwa mbaya mno mjini magenereta kila kona hivi navyondika meseji hii niko gizani sasa unajiuliza tunasonga mbele au tunarudi nyuma
 
Sana yani lakini si anasema kaziba masikio muache atashuhudia mengi kama hili la TANESCO hali imekuwa mbaya mno mjini magenereta kila kona hivi navyondika meseji hii niko gizani sasa unajiuliza tunasonga mbele au tunarudi nyuma
Ukweli ni kwamba tuna rudi nyuma kwa hatua zenye speed kubwa.

Hali hii ya Migao ya umeme tuliishudia kipindi kile cha Kikwete zaidi miaka 10 nyuma.

Walifanya kila mbinu kukabilia na upungufu wa umeme mpaka kipindi cha Magufuli hali ikawa kama imetengamaa .

Gafla bin vuu tupo tena pale tulipo kuwepo 2005

Kama sio kurudi nyuma tuseme nini?
 
Ukweli ni kwamba tuna rudi nyuma kwa hatua zenye speed kubwa. Hali hii ya Migao ya umeme tuliishudia kipindi kile cha Kikwete zaidi miaka 10 nyuma...
Yaani inasikitisha na kuhuzunisha sana

Kila nikitafakari mabwana wale walivyokuwa wakiimba kupewa muda watu walitarajia kutakuwa na mambo mazuri badala yake nchi imeingia kwenye giza la ajabu kuwahi kutokea mpaka ikawafanya mabwana wale kukosoa usingizi na sasa wanafurahia kweli mama abdul kuwahamisha Tanesco

Hivi zile pesa walizopewa kufumua gridi ya Taifa zimefanya kazi gani?
 
Ni bahati sana kwetu kama taifa, bahati mbaya zaidi athari zinakua ni za moja kwa moja kwa mwananchi wa kawaida kama wanavyo tuita!
 
Back
Top Bottom