Hizi Safari za mabasi usiku saa 9, saa 10 ni hatari mno

ubarinolutu

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
2,264
4,702
Naona Sasa ajali za mabasi zimeongezeka Kwa Kasi kubwa sana, hasa haya magari yanayoanza safari kuanzia saa 9 usiku, ni hatari sana.

Serikali inabidi ilihangalie hili, nimejaribu kusafiri mara tatu na haya mabasi ya saa Tisa yaliyotokokea ni haya
1. Safari ya Kwanza tulivyopanda tu gari, baada ya dakika ishirini abiria wote walikuwa wamelala wanakoroma, na hata huko barabarani amani hamna.

2. Katika hizo safari, moja nilichelewa basi kwakuwa nilipitiwa na Usingizi, hata hizo nilizowahi Kuna watu pia walichelewa au kupitiliza, ukiuliza Kila mtu atakuambia ilivyongumu kuamka muda ule na hata ukiamka utakuwa na rundo la usingizi.

3. Mienendo ni mikubwa Kwa madereva, ambao sijui hata kama Wamemaliza usingizi wote, chumba ni kinapea kuliko safari za mchana.

Sasa wadau, serikali iangalie hii ya misafari ya usiku ni hatari, hasa ukiangalia umebeba abiria, Bora miroli ndo itembee usiku.

Hizi Safari hazina tofauti na safari za utalii wa meli za titanic huko chini ya bahati oceanic gate
 
Umetoa sababu za kipuuzi kweli kweli, kwahiyo kwakua unachelewa basi na kulala ukiwa kwenye bus ndio serikali isitishe safari!?

Sema serikali ibadirishe muda wa kuanza,kuanza safari tisa za usiku sijui wanawaza nn,utadhani hawatembei kwenye majiji ya wenzao.

Ukienda kampala bus zinaanza safari kuanzia saa tisa alasiri mpaka saa moja jioni,ukienda nairobi zinaanza kuanzia saa kumi na mbili jioni.

Sasa huu utaratibu hapa kwetu kuanza saa tisa hawaja angalia hata usalama wa wasafiri kutoka makwao mpaka stand.
 
Kwamba huko chini ya bahari oceanic Gate 😁😁😁 ndani ya dk 20 abiria wote wamekoroma 😁😁, badae dereva naye anakoroma mara paap anabwaga gari mtaroni 😁😁 nouma Sana
 
Ukisemea safari za usiku wa saa tisa au saa kumi ndo chanzo Cha ajali kwa nn route ya Dar kwenda Moshi/Arusha au Rombo wanaotoka majira ya saa kumi hawapati ajali mara kwa mara? Swala ni kwamba madereva wachukue tahadhari wanapokuwa barabarani hata ulisema gari zianze Toka saa Moja kama dereva hachukui tahadhari ajali zitaendelea kuwepo
 
Wengi wa mnaopinga usafiri wa usiku mtakuwa vijana wadogo wadogo ambao hamna experience ya kusafiri.

Huko nyuma mabasi yamekuwa yanasafiri usiku na hakukuwa na ajali kama mnavyoona na kuanzisha mijadala.

Safari hizi zilisitishwa kutokana na ujambazi, kupora abilia na kuwafanyia unyama na haikuwa kwa sababu ya ajali, nimesafiri sana na mabasi huko nyuma kwa safari za usiku kutoka Dar kuelekea nje ya mipaka na madereva ni hao hao wawili.

Usiku mkali wa saa 7 bus zima abilia mmelala na kuna ukimya, ni unasikia scania inalalamika tu huko nje na upo seat No. 1 unamuangalia davoo anatafuna bablishi anapiga gear hadi mnafika.

Mfano; kuna madereva wa mabasi ya Scandinavia Express miaka hiyo, namkumbuka Okalla, tulikuwa tunampa tuzo kila mwaka ya udereva bora, kwa taarifa kwenu nyie madogo huyo mwamba (sijui alipo kwa sasa) alikuwa anapiga gear mwaka mzima go and return bila kupumzika, mpaka kampuni inafungwa hajawahi pata ajali.

Mfano mwingine; kuna hizi basi Tawaqal na nyinginezo zinaenda Kongo hadi Zimbabwe unadhani zinalala njiani?.

So issue ya usingizi haisababishwi na eti dereva amefika na kugeuza, No kuna ujinga kwa dereva (labda) kutokuwa makini na kuchukua tahadhari barabarani.
 
Sababu kubwa na chanzo kikubwa Cha ajali ni uchovu na Usingizi, Sasa nyie endeleeni kubisha
 
Naona Sasa ajali za mabasi zimeongezeka Kwa Kasi kubwa sana , hasa haya magari yanayoanza safari kuanzia saa 9 usiku, ni hatari sana.
Serikali inabidi ilihangalie hili, nimejaribu kusafiri mara tatu na haya mabasi ya saa Tisa yaliyotokokea ni haya
1. Safari ya Kwanza tulivyopanda tu gari , baada ya dakika ishirini abiria wote walikuwa wamelala wanakoroma, na hata huko barabarani amani hamna
2. Katika hizo safari , moja nilichelewa basi kwakuwa nilipitiwa na Usingizi, hata hizo nilizowahi Kuna watu pia walichelewa au kupitiliza, ukiuliza Kila mtu atakuambia ilivyongumu kuamka muda ule na hata ukiamka utakuwa na rundo la usingizi
3. Mienendo ni mikubwa Kwa madereva, ambao sijui hata kama Wamemaliza usingizi wote, chumba ni kinapea kuliko safari za mchana.

Sasa wadau , serikali iangalie hii ya misafari ya usiku ni hatari, hasa ukiangalia umebeba abiria, Bora miroli ndo itembee usiku.

Hizi Safari hazina tofauti na safari za utalii wa meli za titanic huko chini ya bahati oceanic gate
Mi nilidhani hatari ni kutokana na ajali kumbe abiria kulala,kuchelewa?
Umelazimishwa kupanda ya usiku?
Tuache tunaopenda mabasi ya usiku tuyafurahie
 
Naona Sasa ajali za mabasi zimeongezeka Kwa Kasi kubwa sana , hasa haya magari yanayoanza safari kuanzia saa 9 usiku, ni hatari sana.

Serikali inabidi ilihangalie hili, nimejaribu kusafiri mara tatu na haya mabasi ya saa Tisa yaliyotokokea ni haya
1. Safari ya Kwanza tulivyopanda tu gari , baada ya dakika ishirini abiria wote walikuwa wamelala wanakoroma, na hata huko barabarani amani hamna.

2. Katika hizo safari , moja nilichelewa basi kwakuwa nilipitiwa na Usingizi, hata hizo nilizowahi Kuna watu pia walichelewa au kupitiliza, ukiuliza Kila mtu atakuambia ilivyongumu kuamka muda ule na hata ukiamka utakuwa na rundo la usingizi.

3. Mienendo ni mikubwa Kwa madereva, ambao sijui hata kama Wamemaliza usingizi wote, chumba ni kinapea kuliko safari za mchana.

Sasa wadau , serikali iangalie hii ya misafari ya usiku ni hatari, hasa ukiangalia umebeba abiria, Bora miroli ndo itembee usiku.

Hizi Safari hazina tofauti na safari za utalii wa meli za titanic huko chini ya bahati oceanic gate
Naenda kupanda Ally's hapa heading Dar soon, hili nalo mkaliangalie.
 
PITA HAPA UPIGE KURA YAKO MKUU

KWA PAMOJA TUNAWEZA KUZUIA AJALI ZA BARABARANI.
 
Wengi wa mnaopinga usafiri wa usiku mtakuwa vijana wadogo wadogo ambao hamna experience ya kusafiri.

Huko nyuma mabasi yamekuwa yanasafiri usiku na hakukuwa na ajali kama mnavyoona na kuanzisha mijadala.

Safari hizi zilisitishwa kutokana na ujambazi, kupora abilia na kuwafanyia unyama na haikuwa kwa sababu ya ajali, nimesafiri sana na mabasi huko nyuma kwa safari za usiku kutoka Dar kuelekea nje ya mipaka na madereva ni hao hao wawili.

Usiku mkali wa saa 7 bus zima abilia mmelala na kuna ukimya, ni unasikia scania inalalamika tu huko nje na upo seat No. 1 unamuangalia davoo anatafuna bablishi anapiga gear hadi mnafika.

Mfano; kuna madereva wa mabasi ya Scandinavia Express miaka hiyo, namkumbuka Okalla, tulikuwa tunampa tuzo kila mwaka ya udereva bora, kwa taarifa kwenu nyie madogo huyo mwamba (sijui alipo kwa sasa) alikuwa anapiga gear mwaka mzima go and return bila kupumzika, mpaka kampuni inafungwa hajawahi pata ajali.

Mfano mwingine; kuna hizi basi Tawaqal na nyinginezo zinaenda Kongo hadi Zimbabwe unadhani zinalala njiani?.

So issue ya usingizi haisababishwi na eti dereva amefika na kugeuza, No kuna ujinga kwa dereva (labda) kutokuwa makini na kuchukua tahadhari barabarani.
Kiongozi usipotoshe Historia, mabasi yalipigwa marufuku kusafiri usiku kwa sababu ya ajali na sio ujambazi.
Mwaka 1992 ajali zilifululiza usiku na kulazimisha PM wa wakati huo Mzee John Malecela kuzuia safari za usiku baada ya Basi la Yarabi Salama kugonga lori lililosimama maeneo ya Ihumwa Dodoma na kuua watu 33.
Hili naomba tusipotoshe historia , baadhi ya mawaziri wasio makini kina Lugola ndio walitumia wongo huo bila kurejea ukweli
 
Nilichopotosha ni kipi labda?.

Historia ipo kwa ajili ya reference na siyo kupinga kitu, but hatuwezi kurudi nyuma kisa ajali iliyotokea miaka hiyo na je ajali nyingi za mchana kweupe ?.

Ndani ya mada mnapinga safari za usiku kisa ajali, alafu unasema usipotoshe mmh!!.
 
Miaka ya 80 na 90 tulikuwa tunasafiri usiku ajali zilikuwepo Marekani ajali zipo Canada ajali zipo Urusi ajali zipo ili gari liwe gari linafungwa fungwa na Bolti na nati elfu moja.
 
Mheshimiwa upotoshaji wako ni Kutoa sababu ya kufungiwa safari za usiku.
Nimesema sio Ujambazi ni Ajali.
hili lieleweke vizuri, sio nakataa safari za usik
 
Saa 9 usiku kuanza safari ni changamoto sana kwa abiria. Yaani kama ndege vile kumbe unawahi Shekilango.
Nashauri safari zianze saa 9 alasiri. Hadi kesho yake saa 2 mtu yuko Mwanza.
 
Back
Top Bottom