Kwa hakika suala la kuhifadhi pesa ili nifanyie uwekezaji imekua ni suala gumu sana kwangu kwani kila nikiwa na kiwango fulani cha fedha kwenye akaunti nakuwa na msukumo mkubwa wa kutumia hiyo pesa hata kabla sijatimiza malengo yangu...kwa hiyo ninabaki kuwa mtu wa mipango tu kipindi sina ila nikipata fedha nakuwa sijui hata imeishaje. Tupeane uzoefu namna ya kujibana na kupunguza nguvu zinazokushawishi kutumia pesa sehemu ambayo hukupanga kutumia ....hii pesa sijui ina nini wakuu ebu tupeane uzoefu wa matumizi mazuri kwani natamani kuweka akiba na kuwekeza, na kwangu pesa inapatikana ila sasa matumizi yanavyozuka hata sijui yanatokea wapi.