Hivi watu wanaosubiri kutekelezwa kwa hukumu ya kifo, siku au dakika za mwisho huwa wanakuwa katika hali gani?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,671
149,843
Kuna jambo limenikumbusha vita ya ghuba(Second Persian Gulf war) ile iliyomuondoa madarakani aliekuwa Raisi wa Iraq, Bwana Saddam Hussein. Nikakumbuka huyu bwana alihukumiwa adhabu ya kifo kwa kunyongwa hadi kufa.

Saddam ni mfano tu wa watu wengi waliouwawa kwa adhabu ya kifo iwe kwa kunyongwa, kuchomwa sindano ya sumu, n.k.

Swali ninalijiuliza, watu hawa wanaosiubiri kutekelezwa kwa adhabu za kifo, huwa wanakuwa na hali gani dakika za mwisho?

Na je, ndugu zao nao huwa na hali gani?

Hakika hii adhabu ni mbaya sana isipokuwa kwa wale wanaoamini wanahukumiwa kufa kwasababu walipigania jambo kwa imani ya misingi ya kidini(wanakuwa na matumaini kuwa wanafia dini yao yaani Mungu) au wale wanaomani wanakwenda kufa kishujaa, tofauti na hapo, ni mateso mabaya sana ya kisaikolojia na sijui kama hujwa wanapata usingizi siku zikikaribia.
 
Kwahuko kwenu sijui, ila huku Udanganyikani nakoishi mimi huwa hawanyongwi labda wale wa kesi za uhaini au ugaidi wa mass destruction. Kwa wazee na wagonjwa wanaachwa wafe natural deaths, kwa vijana wenye nguvu kuna spesho trainings wanafanya ambazo zinasaidia nchi kwenye maeneo fulani fulani. Ila ndo hamtawaona tena uswazi.
 
Ukienda pale karibu na Mahakama ya Kisutu, kuna Archive, inatunza kumbukumbu nyingi pamoja na kumbukumbu zote za death penalty tangu enzi ya mjerumqni, declassifed documents, though kuingia zengwe tu kama kawaida ya nchi zenye mlengo wa mashariki.

Horrifying stories, hapo kuna stories hata kwa nini wazungu waliamua kukabidhi jukumu la kunyonga kwa waafrika baada ya incident moja ya kutisha kutokea, na ikaripotiwa kwa gavana wa kijerumani
 
Sana sana ni regrets za aliyoyafanya na ambayo hakuyafanya, uwoga wa mateso ahisiyo atayapitia kabla ya kufa na zaidi ni maswali ya kwamba nini kitafuata baada ya pumzi yake kukatika.

Kuna video moja nilishawahi kuiona jamaa alikua anapewa lunch yake ya mwisho kabla ya kuuwawa alikua anakula kwa kutetemeka huku akiwa na wasiwasi sana…. Lakini ukiachilia hayo kuna mgonjwa akifika stage flani anajua kabisa kwamba muda wowote kuanzia sasa kipenga kinalia.

Japokua mjomba Saadam alikua anatabasamu.
 
Hukumu mbaya kuliko zote ni ile ya electric chair bora hizo nyingine, by the way hilo swali tuwaulize pia na wale wagonjwa wa cancer stage ya mwisho, ambao wanakuwa wanajua kabisa kwamba baada ya muda fulani they will be no more
Same thing hata kwa wasiokua na cancer, kwasababu hata sisi hatuna uhakika wa dakika ifuatayo hata kama afya zetu zipo imara…
 
Kwa nchi kama USA ambayo inatekeleza hukumu hiyo, siku ya mwisho mfungwa anaagiza last meal chakula anachopenda , anatenganishwa na wenzake, na muda mfupi kabla ya kutekelezwa kwa hukumu anaoga fresh lakini pia hukumu huwa inatekelezwa usiku
 
Same thing hata kwa wasiokua na cancer, kwasababu hata sisi hatuna uhakika wa dakika ifuatayo hata kama afya zetu zipo imara…
Teodore Bagwell aka T-Bag one of my fav movie character, sio kweli. Kwa wenye imara imara utaendelea kupanga mipango yako ya future kama kawaida simply because you are not aware how soo or later you gonna die. Kwa wale wanaojua wakati wao what they do is not future planning but regrets, fear, repenting, worries, loosing hope and sometimes mare hopes.
 
Kwa nchi kama USA ambayo inatekeleza hukumu hiyo, siku ya mwisho mfungwa anaagiza last meal chakula anachopenda , anatenganishwa na wenzake, na muda mfupi kabla ya kutekelezwa kwa hukumu anaoga fresh lakini pia hukumu huwa inatekelezwa usiku
Bado haisaidii mkuu, sema basi tu.
 
Back
Top Bottom