Hivi ndiyo kusema mgodi wa Mwadui umetoa pesa kiasi hiki!?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
8,468
14,960
Wakati wa kutekeleza Azimio la Arusha serikali ilichukua hisa asilimia 50 za mgodi wa Mwadui. Sasa ikaonekana wafanyakazi wa serikali mgodini pale wanalipwa pesa nyingi sana na Nyerere alitaka kuweka usawa katika kipato cha watanzania. Basi wakataka kuwashushia mshahara na wakapanga wapate ngapi.

Jamaa wakasema huo mshahara utakuwa ni mdogo mno ukilinganisha na posho tuliyokuwa tunalipwa wakati wa mafunzo ya kazi za mgodini kwa siku. Nyerere akakiri kwamba walitaka kufanya jambo la ajabu.

Nimeona wikipedia kuwa toka mgodi wa Mwadui uanze uzalishaji hadi leo umezalisha kilo 3800 za almasi. Leo hii bei ya chini ya almasi ni Tsh milioni 10 kwa gram. Kilo moja ya almasi ni bilioni 10!! Kilo 3800 ni trilioni Tsh 38. Hizi hesabu za haraka haraka na simple. Kuna nchi zina mali dunia hii!!
 
Kama ni kweli bas huo mgodi sio sana, mana kama umezalisha T38, hapo hujaweka cost ya uzalishaji, tuseme dhahabu profit ni 50% means toka uanze faida ni T19, bas ni ndogo mana toka kipind cha nyerere upo, so hio hela ukigawanya kwa hio miaka duuuh,
Lazima kiasi kikubwa kinatoroshwa
 
Back
Top Bottom