Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,409
- 13,260
Sijui watu wa aina hii wanajisikiaje wanapojitambulisha kuwa na elimu kubwa kama Phd, Uprofesa, Uinjinia na ubobevu katika masuala fulani halafu kiutendaji, uelewa wa mambo, busara, hekima na lugha wanakuwa chini sana kulko wenye elimu ndogo mathalani ya darasa la saba, sekondari au hata digrii moja. Nikiangalia baadhi ya viongozi wetu wanapenda sana kujionesha kuwa ni wasomi lakini kusema kweli ni majina tu lakini uwezo ni mdogo sana. Katika nchi nyingi sana duniani ikiwemo zile zilizoendelea kiuchumi na kiteknolojia huwezi kukuta viongozi wao wakijitambulisha kwa vyeo vyao vya kielimu za kusoma na kupewa kama Dr, Prof, Eng, nk lakini wabongo wanavyopenda sifa! Ukijitambulisha kwa elimu kubvwa lazima watu waone uwezo wako kivitendo, hekima na busara.
Ingekuwa vizuri sasa wapenda sifa hao wawe wanaweka kabisa CV zao zikionesha jinsi walivyofaulu huko shuleni na vyuoni. Mfano kiongozi aweke wazi matokeo yake ya Sekondari Kidato cha nne na sita tuone ufaulu wake katika kila somo alipata nini. Vile vile katika ngazi ya chuo kikuu na vyuo vingine aweke Transcript yake tuone alifanya nini na alipata Class gani. Tukifika kwenye Phd na Uprofesa pia tuone walibobea katika nini na walipataje kufika ngazi hizo kama vigezo na masharti vilizingatiwa. Tukifikia hapo huu ujanja ujanja wa kujiita Dr, Prof. na Eng, utaisha. Ukiwaangalia VP na PM utagundua wako vizuri sana kulinganisha na wenye mikwara ya uprof na Phd. Hotuba zao huwa zinakuwa za kitaifa zaidi bila ubaguzi wala kuleta mitafaruku huwa wanajitahidi sana kutenganisha shughuli za kiserikali na chama na huwa wametulia sana