Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,121
- 39,233
Watanzania na dunia tumekuwa tukipewa taarifa mbili tofauti za visa vya Corona kutoka katika taifa la Tanzania (Tanganyika na Zanzibar) huku wakati mwingine kukiwa na mchanganyo wenye kutupa wasiwasi au marudio ya taarifa zile zile pasipo sababu ya msingi.
Waziri wa Afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu amekuwa akitoa taarifa za Corona kwa Tanzania nzima (ikiwemo Zanzibar) na wakati huo huo Waziri wa Afya wa Zanzibar, Hamad Rashid akitoa taarifa za Corona kwa Zanzibar.
Ni kweli tunajua suala la Afya sio suala la muungano, hivyo Zanzibar wako sahihi na wanayo haki ya wao kulisemia bila mamlaka za serikali ya muungano kuwaingilia, lakini busara ingeweza kutumika kwa suala hili kubakia kusemewa na waziri wa Tanzania tu ili kuepusha mchanganyo wa kitaarifa kwa dunia inayofuatilia suala hili kwa karibu mnoo.
Upande wa pili ni kuwa, kwa kuwa la suala la Afya sio la muungano, ingekuwa ni busara kwa waziri wa muungano wa Tanzania kuwasemea watanzania bara tu na kuwaacha wazanzibar wao wenyewe kulisemea maana halimhusu.
Busara ianze kutumika sasa, huko tunakoelekea ipo hatari ya mmoja kumharibia mwingine taarifa zake pasipo kukusudia.