IPECACUANHA
JF-Expert Member
- Feb 19, 2011
- 3,224
- 1,914
Katika kukazia katika nidhamu hilo liko sawa ilisemwa "ahadi ni deni "Kuna mtu aliandaa sherehe ya arusi lakini ili kufanikisha sherehe akaitaji michango toka kwa ndugu na marafiki.
Kwa kuwa alikua maarufu sana watu mbalimbali walijitokeza kumchangia ili afanikishe hiyo harusi.
Wengine walitoa cash wengine ahadi, michango ilipozidi kumiminika akabadili gia angani akaanza kujenga Nyumba yake binafsi, waliokwisha kuchanga wakawa wanashangaa make hakuficha aliwaambia kuwa michango imekua mingi na bado kuna watu wameahidi kuleta, hivyo hizi zilizotangulia nimeona nijenge nyumba.
Baada ya mda akaona wale walioahidi hawaleti michango yao, sasa kawatangazia kuwa lazima ile michango itolewe.
Hivi ni sahihi kumlazimisha mchangiaji atoe ahadi yake wakati anaona michango ya waliotangulia haikulenga kusudio la kuchanga??