Hivi imeshindikana kabisa kuwa na maeneo maalumu ya kuegesha Malori badala ya pembeni ya Barabara?

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,591
8,810
1707045633902.png

Moja kati ya sababu za ajali za kila wakati katika Barabara kuu nchi hii ni Malori yanayoegeshwa bila utaratibu maalum kwenye Barabara za pembeni ambazo mara nyingi hutumika na waenda kwa miguu, dharura za hapa na pale. Lakini cha ajabu ni kama suala hilo linakuwa kawaida na linaachwa liendelee kuota mizizi hasa katika majiji makubwa kama Dar.

Barabara nyingi za Dar zimegeuka kuwa Parking za Malori ambayo ni aidha yanasubiri Mizigo, madereva wanapumzika au kufanya matengenezo ya kihuni huni tu.

Malori haya yamekuwa chanzo cha msongamano mkubwa magari na kuchelewesha huduma za usafiri kwa magari mengine na watumiaji wa barabara hizo. Mfano kutoka Ubungo kwenda Buguruni barabara za pembeni zinajazwa Malori kila siku. Hivi kwanini Mipango miji hawafikirii kutumia fursha hiyo kutenga maeneo angalia kila baada ya kilomita 10 kuwe eneo la Malori kupaki na isiwe karibu na Barabara kuu ili kuondoa kero hiyo.

Ifike wakati Serikali ione mambo kwa macho ya ziada.
 
Mizigo itakuwa yachukuliwa Kwala hivyo magari yatapungua kuja mjini kasoro ya Mafuta tu
 
Shida ni utekelezaji na ufatiriaji wa namna ya kutekeleza..!

Mfano kahama kuna parking kubwa ya malori ajabu, unakuta maroli pembezoni ya balabala na parking ipo!

Hapo ndo inabidi kuamini tuna miaka sii chini ya mia ya kubadili mitizamo yetu, na mamlaka kusimamia hiyo mitizamo!
 
Back
Top Bottom