mpita-njia
JF-Expert Member
- Dec 3, 2010
- 1,734
- 1,615
Wakuu nimekaa najiuliza sana kutokana na Sakata linaloendelea,
1.Swali ili uwe mkuu wa mkoa yakupasa kuwa na Elimu kiwango gani?
2. Nafasi ya mkuu wa mkoa inasomewa au ni yakuteuliwa tu kwa utashi wa kiongozi aliye madarakani kuona kwamba huyu mtu atanisaidia kwenye 1,2,3
3. Kwanini watz tunapiga Sana kelele kuhusu Elimu ya Mheshimiwa Makonda huku tukijua ni nafasi ya kuteuliwa?
4. Ukaguzi wa vyeti fake ulikuwa unalenga wafanyakazi wa namna gani?
5. Hivi ni kweli watz hatuna shughuli ya kufanya kabisa?
Naomba mwenye uelewa anijuze nipate kuelewa naomba kuwasilisha.
NB: mods nawaona tu...
Mfano tu rahisi achilia mbali mambo ya Madawa.
Iqbal kampa bwana yule ardhi bure.
Badala ya kwenda kwenye vitengo husika kufuatilia badala yake kaita waandishi wa habari Kigamboni kukabidhiwa eneo na bwana Iqbal.
Leo imejulikana kama kesi ilikuwa mahakamani na huyo Iqbal ameshindwa, wizara ilikuwa kwenye precess ya kuwarudishia wananchi ardhi yao.
Yaani full kukurupuka ili kupata headlines.