Wakuu,
Ukifanya kosa/makosa ya usalama barabrani unaandikiwa karatasi inayojulikana kama notification amabayo unalipia na baadaye unaenda kudai risiti kwa Mhasibu wa Polisi. Na kama utazidisha muda maalum wa kuwasilisha hiyo documents uwezi kukatiwa risiti kwa maana pesa inakuwa imeliwa.
Swali la kujadili: Hizi pesa baada ya kupita muda huo siku tatu wakati umeishalipa huwa zinawekwa kwenye mfuko upi wakati hazijapokelewa rasmi na stakabadhi ya serikali?
Hivi kwanini Traffic wasitoe stakabadhi za kielectronic.
Notification hizi zimeandikwa kwa kiingereza kwanini zisiandikwe kwa kiswahili? Kwa maana wengi wanaopewa karatasi hizi hawajui hata kusoma hiyo lugha.
NB: Kuna wizi mkubwa sana katika hii idara ya polisi usalama barabarani kwani wakati mwingine wanafanya makusudi na wakati mwingine wanadiriki hata ku backdate tarehe ili ukienda kuomba risiti wakwambie muda umeisha wa notification.