Hivi hili gorofa limefikia hatua ya mwisho serikali ilikuwa wapi?

bado natafakari litabomolewa kwa style gani?


Kwa kawaida huchimbiwa baruti za kutosha katika mihimili ya jengo kuanzia chini mpaka juu halafu hulipuliwa hizo baruti kwa mpangilio maalumu,ikiwa jengo linaangukia upande wa kusini basi baruti za kaskazini hulipuliwa vivyo hivyo kwa mashariki na magharibi.

Ni utaalamu ambao watu wameubobea,kwa kuanzia serikali inaweza kutangaza yenda kwa makampuni yanayofanyazi kazi hizo dumiani hasa kule kwenye matetemeko ya mara kwa mara. Majumba yaliyobomoka nusu humaliziwa kwa mtindo huu.
 
Ttulikuwa hatuna serikali miaka kumi iliyopita.
Ivi tanzania kuna serikali?? ishawahi kuwepo?? ipo?? na wewe unaamini ipo hiyo serikali?? mimi siamini na siamini kama ilikuwepo au ipo ama itakuwepo sio leo wala kesho!!
 
mmh ila hilo jengo kwa kuliangalia tu linatisha..ni kama halina balance ya kueleweka hivi..!!watu walikuwa wanapandisha tu kama wanapanga viberiti..!!
Logistics za kulibomoa Ni ngumu kuliko kulijenga. Hebu angalia nafasi iliyopo kati ya hili jengo na majirani. Labda wateremshe tofali moja moja kutoka juu. Maajabu mengine haya!
 
Tuliruhusu wanasiasa kuwa na nguvu kuliko wataalam huku yule mkwere wa Msoga akiiacha nchi kwenye autopilot. Hii itakuwa fursa nzuri sana kwa watanzania kwa miaka mingi ijayo kuelewa umuhimu wa kufuata sheria
Hata autopilot iko vizuri mkuu, ndege ukiacha kwenye auto pilot haipati ajali kizembe, ni very intelligent ile kitu
 
Mmiliki wa gorofa hilo ni nani?nahisi mpaka sahvi atakuwa amelazwa kwa kupatwa na presha....?
Maji ya kifuu bahari ya Chungu!
Athari kwa mmiliki wa Hilo jengo zaweza kua ndogo kuliko mtu alievunjiwa nyumba ya chumba kimoja Kwenye bonde la Msimbazi !
 
Iliamrishwa ibomolewe soon baada ya pacha yake kuporomoka yenyewe na kuua dozens of people! Lkn cha ajabu na kwa ujeuri na kiburi wakaendelea na ujenzi! Sasa tuone hatua stahiki zinachukuliwa kuokoa life za wanadamu
 
Wabomoe tu hamna namna. Ila hawa wanaotoa vibali huwa hawakagui maendeleo ya majengo kabisa huu ni uzembe
 
Back
Top Bottom