Hivi hii imekaaje mwanaume kuvaa kanga na kujionyesha nayo nje?

Wote mliochangia hapo juu hamjui utamu wa mke na hamjaoa.Nina mataulo ya kutosha ila w end mke wangu anapenda nivae kitenge
Sasa kwenye utamu wa mke kanga ndo uvae nje huku mjegejo upo mbashara kwenye kanga
 
"Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi yampasayo mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako". TORATI 22:5.

Na hilo ndilo Neno la Mungu.
 
Wengi bado watoto humu .. hawajui utamu wa mke hata kama wameoa bila shaka hawa wanaona ajabu mwanaume kuvaa kanga ni vijana wa siki hizi ..
 
Sasa kwenye utamu wa mke kanga ndo uvae nje huku mjegejo upo mbashara kwenye kanga
Mkuu oa kwanza na nyinyi wanaume wa mikoani mnaishi na wake zenu kibabe hata wanakuwa sio wabunifu wanawaogopa mm w end sivai tauro mke wangu anasema zito ni mwendo wa kitenge
 
Hivi mtu anayevaa Kanga ya mke wake hana uwezo wa kununua Taulo?Hivi niwe na uwezo wa kuanza kujenga vyumba viwili nishindwe kununua Taulo?
"Wauza mataulo msipite ninapokaa kupitisha mataulo,kanga ya mke wangu inanitosha maana inapitisha upepo mpaka kumoyo"
 
Safi sana mkuu mpende sana mkeo huyo ndio wa maisha yako.hawa wahuni hawana wake wanachangia mambo ya kaka zao
Si kwasababu tunawalea, kwahiyo ukitoka umevaa kitenge inajulikana kumbe baba mle ni yule. Na wenyewe si wanauzaga CD aaah pale nimepanga ubavu, ***** zao.
 
Ajakuomba uvae dera

Ukivaa khanga ina maana umeoa.

Daima huwezi kuwa na khanga ndani ya nyumba kama huna mke.

Acheni utoto. Tuulizeni wenye familiya tunajua.

SEMA USIKIKE.....

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
leo kimenuka mapemaa bora single mothers wapumue leo
Vipi miss anavaaga kanga ukiwa naye? Hebu tupe uzoefu wa uliyempata
Ukishajibu umuombe mode akubadilishe jina maana ulitwambia ulishapata
Napendekeza
Miss nshapata mume
Miss nilipata
Miss ninaye tayari
N.k
 
"Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi yampasayo mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako". TORATI 22:5.

Na hilo ndilo Neno la Mungu.
Amen
 
watu wa bara mambo ya watu wa pwani yaachane hivohivo... nyie si mmezoea kuvaa ngozi ya ng'ombe
 
Mbona nina mwaka wa 5 kwenye ndoa na nampenda sana mke wangu ila kanga sijavaa mkuu, kila kitu kina utaratibu na kanuni zake kaka mwisho atakuvalisha dela
NINA MIAKA 21 KATIKA NDOA, TOKA MWAKA 1996 LAKINI KHANGA KILA NIENDAPO KUOGA NDO VAZI LANGU, NIKIVUA ANAVAA MKE WANGU.

SEMA USIKIKE.....


MIZAMBWA
INANUMA SANA!!!!
 
mbona kawaida sana ukienda kuoga unavaa kanga ya wife kwani kuna ubaya gani? naona wanaobisha bado wapo shule hawajui mahaba ya ndoa kwa wawili wapenda nao
 
Ukivaa khanga ina maana umeoa.

Daima huwezi kuwa na khanga ndani ya nyumba kama huna mke....
Hapa nakupinga, mtu unakua nazo kwa sababu mwenzako anaweza kuja na hiyo ndiyo atakayoshindia.
 
Back
Top Bottom