Kwa uelewa wangu mdogo najua state au nchi ina mihimili yake mitatu ambayo inajitegemea na kujisimamia bila mwingine kuingilia utendaji wa mwingine.
Mihimili hii ni Serikali, Bunge ambalo husimamia serikali na kutunga sheria na wa tatu ni mahakama ambayo hutafsiri sheria.
Nashangazwa na kitendo cha leo bunge kuwa live asubuhi na jioni hii naamini litakuwa live kupitia tbc kwa kuwa tu ni serikali inaongea au kwa maneno mengine ni serikali inawasilisha taarifa ( bajeti).
Hii imekuwa kawaida kwa kipindi cha maswali na majibu kwani mawaziri ( serikali) ndio waongeaji na wasemaji.
Mjadala wa kukosoa serikali kwa inachofanya au kuwasilisha unazuiliwa eti watu hawatafanya kazi. ( saa moja na nusu asubuhi hadi saa tisa na nusu alasiri) sasa bunge kama mhimili unaojisimamia inakuwaje lipo tayari kuonesha na kutangaza serikali badala ya bunge lenyewe?
Muda wote waziri wa fedha yupo hewani, lakIni majadiliano ya serikali ilichokileta hawaoneshi. Sio sahihi.
Au leo watu hawajafanya kazi ilikuwa siku ya mapumziko. Na je bunge kikao ni saa tatu hadi saa sita muda huo ndio watu hawatafanya kazi.
Tanzania na demokrasia ipo safari ndefu sana