Hitler alipisha Meli na Majeshi Uingereza (english channel) bila ya Kugundulika!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Ulishawahi kuisikia habari hii kwamba wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia ambapo kwa Ulaya ilikuwa ni Ujerumani chini ya Adolf Hitler na marafiki zake kama Italia dhidi ya Urusi, Uingereza na baadaye Marekani kuja kuokoa jahazi, Adolf Hitler alipitisha Meli zake za kivita kama cruiser Prinz Eugen kutoka Koloni lake la Ufaransa ambako walikuwa wameshakuteka kupitia uchochoro wa wa bahari ya Uingereza (English channel) mpaka kwao Ujerumani kwenye kile kilichoitwa Operation Cerberus bila kugundulika ingawaje Waingerea walikuwa wamewekeza kila kitu kwenye kulinda English channel lkn Meli za Kivita za Manazi zilipita bila mtu yoyote yule kugundua yaani kama vile Meli za Kivita za adui zipite Kigamboni kwenye bahari yetu kuelekea Msumbiji bila ya sisi kugundua!

Hii inaitwa ndiyo one of the best military maneuver ever kwa maana meli za kivita zimepita usoni mwa ulinzi na Radar na kila kitu cha Uingereza bila kugundulika walikuja kugundua na kuanza kurusha Makombora wakati Meli za Adolf Hitler zilishapita na kuvuka English channel!

Ramani chini inaonyesha uchochoro wa Bahari ya Uingereza (English Channel) ambapo Hitler alipitisha Meli zake za Kivita kuzirudisha kwao Ujerumani kutokea Koloni lake la Ufaransa mpaka kwao Ujerumani bila ya kugundulika na Majeshi ya Uingereza ingawaje yalikuwa yanalinda uchochoro wa Uingereza kwa makini kupita kiasi!



Channel Dash - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Mpwa alitumia teknolojia gani? Hebu ongeza nyama kidogo


Manazi ndiyo baba wa modern Warfare yote leo hii hapa Duniani, hivyo ni kwamba walikuwa mbele kiteknolojia na ndiyo maan walishindwa kuwadetect kwa kama ni radar Manazi walikuwa nazo advanced zaidi!"
 
Apite katika radar asionekane? Meli ya kivita ipite kigamboni kwa macho isionekane na katika radar pia..Mrusi aligusa kidogo tuu anga za Mturuki na ndege yake kilichowapata mpaka sasa hawafanyi biashara..izo ni hadith tuu Nyambizi tuu inaonekana sembuse Meli..
 
Vitani chochote chawezatokea. Vita ni kama mchezo wa mpira. Ni timingin, ushushu, umafya n.k.

Usikute jamaa alishapenyesha watu wake ndani ya Uingereza na kukorofisha mitambo ili jamaa wapite (special operations by psecial forces)

Kwani hujasikia B52 yenye stealth tech ya USA ilitunguliwa ktk vita ya Serbia kwa komboro tena la kizamani? Inasemekana, Serbia walisaidiwa na Warusi kuingilia maswaliano baina ya USA na washirika wake wa EU na kupata njia na mida ya dege hilo nahivyo kulitungua kirahisi.
 
Adolf Hitler is full of surprises, sipatipicha Dunia ingekuaje kama mipango yake ingekamilika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…